Isaiah 1:23 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Viongozi wako ni waasi; wanashirikiana na wezi. Kila mmoja anapenda hongo, na kukimbilia zawadi. Hawawatetei yatima, haki za wajane si kitu kwao.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Watawala wenu ni waasi, rafiki wa wezi, wote wanapenda rushwa na kukimbilia hongo. Hawatetei yatima; shauri la mjane haliletwi mbele yao.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Wakuu wako ni waasi, na rafiki za wevi; kila mtu hupenda rushwa, hufuata malipo; hawampatii yatima haki yake, wala maneno ya mjane hayawawasilii.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Viongozi wako ni waasi; wanashirikiana na wezi. Kila mmoja anapenda hongo, na kukimbilia zawadi. Hawawatetei yatima, haki za wajane si kitu kwao.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Watawala wenu ni waasi, rafiki wa wevi, wote wanapenda rushwa na kukimbilia hongo. Hawatetei yatima, shauri la mjane haliletwi mbele yao likasikilizwa.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Watawala wenu ni waasi, rafiki wa wevi, wote wanapenda rushwa na kukimbilia hongo. Hawatetei yatima, shauri la mjane haliletwi mbele yao lisikilizwe.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Wakuu wako ni waasi, na rafiki za wezi; kila mtu hupenda rushwa, hufuata malipo; hawampatii yatima haki yake, wala maneno ya mjane hayawafikii.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Viongozi wako ni waasi; wanashirikiana na wezi. Kila mmoja anapenda hongo, na kukimbilia zawadi. Hawawatetei yatima, haki za wajane si kitu kwao.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Wakuu wako hufanya fujo, wenzao ni wezi, wao wote hupenda matunzo, hufuata fedha za kupenyezewa, wafiwao na wazazi hawawaamulii, wala mashauri ya wajane hayafiki kwao.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Wakuu wako ni waasi, na rafiki za wevi; kila mtu hupenda rushwa, hufuata malipo; hawampatii yatima haki yake, wala maneno ya mjane hayawawasilii.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Wakubwa wako ni waasi; wanashirikiana na wizi. Kila mumoja anapenda kituliro, na kukimbilia zawadi. Hawamupatii yatima haki yake, haki za wajane si kitu kwao.