Isaiah 1:24 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Kwa hiyo asema Bwana Mwenyezi-Mungu, Mwenye Nguvu wa Israeli: “Nitawamwagia maadui zangu hasira yangu, nitawalipiza kisasi wapinzani wangu.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Kwa hiyo Mwenyezi Mungu, Mungu wa majeshi ya mbinguni, Mwenye Nguvu wa Israeli, asema hivi: “Lo! Nitapata faraja kutoka kwa adui zangu, na kujilipizia kisasi kwa watesi wangu.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Kwa hiyo, asema Bwana, Bwana wa majeshi, Mwenye enzi, wa Israeli, Nitapata faraja kwa hao wanipingao, nitatwaa kisasi kwa adui zangu;
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Kwa hiyo asema Bwana Mwenyezi-Mungu, Mwenye Nguvu wa Israeli: “Nitawamwagia maadui zangu hasira yangu, nitawalipiza kisasi wapinzani wangu.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Kwa hiyo Bwana, BWANA Mwenye Nguvu Zote, Mwenye Nguvu wa Israeli, asema hivi: “Lo, nitapata faraja kutoka kwa adui zangu na kujilipizia kisasi juu ya watesi wangu.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Kwa hiyo Bwana, bwana Mwenye Nguvu Zote, Mwenye Nguvu wa Israeli, asema hivi: “Lo, nitapata faraja kutoka kwa adui zangu na kujilipizia kisasi juu ya watesi wangu.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Kwa hiyo, asema Bwana, BWANA wa majeshi, Mwenye enzi, wa Israeli, Nitapata faraja kwa hao wanipingao, nitalipiza kisasi kwa adui zangu;
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Kwa hiyo asema Bwana Mwenyezi-Mungu, Mwenye Nguvu wa Israeli: “Nitawamwagia maadui zangu hasira yangu, nitawalipiza kisasi wapinzani wangu.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kwa sababu hiyo ndivyo, asemavyo Bwana, yeye Bwana Mwenye vikosi amtawalaye Isiraeli: Patafika, nitakapojituliza kwao wapingani wangu, nikiwalipiza adui zangu!
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Kwa hiyo, asema Bwana, BWANA wa majeshi, Mwenye enzi, wa Israeli, Nitapata faraja kwa hao wanipingao, nitatwaa kisasi kwa adui zangu;
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Kwa hiyo, nitawamwangia waadui zangu hasira yangu, nitawalipiza kisasi wapinzani wangu. –Ni ujumbe wa Bwana wetu Yawe wa majeshi, Mwenye Nguvu wa Israeli.–