Isaiah 1:4 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Ole wako wewe taifa lenye dhambi, watu waliolemewa na uovu, wazawa wa wenye kutenda maovu, watu waishio kwa udanganyifu! Nyinyi mmemwacha Mwenyezi-Mungu, mmemdharau Mtakatifu wa Israeli, mmefarakana naye na kurudi nyuma.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Ole wa taifa lenye dhambi, watu waliolemewa na uovu, uzao wa watenda mabaya, watoto waliozoelea upotovu! Wamemwacha Mwenyezi Mungu, Wamemkataa kwa dharau yeye Aliye Mtakatifu wa Israeli na kumgeuzia kisogo.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Ole wake, taifa lenye dhambi, watu wanaochukua mzigo wa uovu, wazao wa watenda mabaya, watoto wanaoharibu; wamemwacha Bwana, wamemdharau yeye aliye Mtakatifu wa Israeli, wamefarakana naye na kurudi nyuma.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Ole wako wewe taifa lenye dhambi, watu waliolemewa na uovu, wazawa wa wenye kutenda maovu, watu waishio kwa udanganyifu! Nyinyi mmemwacha Mwenyezi-Mungu, mmemdharau Mtakatifu wa Israeli, mmefarakana naye na kurudi nyuma.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Lo! Taifa lenye dhambi, watu waliolemewa na uovu, uzao wa watenda mabaya, watoto waliozoelea upotovu! Wamemwacha BWANA, Wamemkataa kwa dharau yeye Aliye Mtakatifu wa Israeli na kumgeuzia kisogo.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Lo! Taifa lenye dhambi, watu waliolemewa na uovu, uzao wa watenda mabaya, watoto waliozoelea upotovu! Wamemwacha bwana, Wamemkataa kwa dharau yeye Aliye Mtakatifu wa Israeli na kumgeuzia kisogo.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Ole wake, taifa lenye dhambi, watu wanaochukua mzigo wa uovu, wazao wa watenda mabaya, watoto wanaoharibu; wamemwacha BWANA, wamemdharau yeye aliye Mtakatifu wa Israeli, wamefarakana naye na kurudi nyuma.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Ole wako wewe taifa lenye dhambi, watu waliolemewa na uovu, wazawa wa wenye kutenda maovu, watu waishio kwa udanganyifu! Nyinyi mmemwacha Mwenyezi-Mungu, mmemdharau Mtakatifu wa Israeli, mmefarakana naye na kurudi nyuma.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Utaona, wewe kabila lenye makosa, nanyi mnaolemewa na manza, mlizozikora, wewe kizazi cha wabaya, nanyi wana wapotovu! Wamemwacha Bwana na kumbeza Mtakatifu wa Isiraeli, wakarudi nyuma.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Ole wake, taifa lenye dhambi, watu wanaochukua mzigo wa uovu, wazao wa watenda mabaya, watoto wanaoharibu; wamemwacha BWANA, wamemdharau yeye aliye Mtakatifu wa Israeli, wamefarakana naye na kurudi nyuma.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Ole kwako wewe taifa lenye zambi, watu waliolemewa na uovu, kizazi cha watenda mabaya, watoto wanaoishi kwa udanganyifu! Ninyi mumemwacha Yawe, mumemuzarau Mutakatifu wa Israeli, mumerudi nyuma.