Isaiah 1:6 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Toka wayo hadi kichwa hamna penye nafuu, umejaa majeraha na vidonda vitoavyo damu, navyo havikuoshwa, kufungwa wala kutiwa mafuta.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Kutoka wayo wako wa mguu hadi kwenye utosi wa kichwa chako hakuna uzima: ni majeraha matupu na makovu na vidonda vinavyotoa damu, havikusafishwa au kufungwa wala kulainishwa kwa mafuta.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Tangu wayo wa mguu hata kichwani hamna uzima ndani yake; bali jeraha na machubuko na vidonda vitokavyo usaha; havikufungwa, havikuzongwa-zongwa, wala havikulainishwa kwa mafuta.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Toka wayo hadi kichwa hamna penye nafuu, umejaa majeraha na vidonda vitoavyo damu, navyo havikuoshwa, kufungwa wala kutiwa mafuta.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Kutoka wayo wako wa mguu hadi kwenye utosi wa kichwa chako hakuna uzima: ni majeraha matupu na makovu na vidonda vitokavyo damu, havikusafishwa au kufungwa wala kulainishwa kwa mafuta.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Kutoka wayo wako wa mguu hadi kwenye utosi wa kichwa chako hakuna uzima: ni majeraha matupu na makovu na vidonda vitokavyo damu, havikusafishwa au kufungwa wala kulainishwa kwa mafuta.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Toka wayo wa mguu hadi kichwani hamna uzima ndani yake; bali jeraha na machubuko na vidonda vitokavyo usaha; havikufungwa, havikuzongwazongwa, wala havikulainishwa kwa mafuta.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Toka wayo hadi kichwa hamna penye nafuu, umejaa majeraha na vidonda vitoavyo damu, navyo havikuoshwa, kufungwa wala kutiwa mafuta.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Toka wayo wa mguu mpaka kichwani hapana palipo pazima, ni madonda na machubuko na mapigo matupu; hayaoshwi, wala hayakufungwa, wala hayakulegezwa na mafuta.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Tangu wayo wa mguu hata kichwani hamna uzima ndani yake; bali jeraha na machubuko na vidonda vitokavyo usaha; havikufungwa, havikuzongwa-zongwa, wala havikulainishwa kwa mafuta.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Tokea kwenye muguu mpaka kwenye kichwa hakuna chenye kuwa kizima; ni machubuko, alama za mapigo na vidonda vinavyovuja damu, vilivyokosa kusafishwa, kufungwa wala kutulizwa kwa mafuta.