Isaiah 10:12 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Wakati Mwenyezi-Mungu atakapomaliza kazi zake zote mlimani Siyoni na mjini Yerusalemu, atamwadhibu mfalme wa Ashuru, kwa sababu ya majivuno na kiburi chake.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Bwana atakapokuwa amemaliza kazi yake yote dhidi ya Mlima Sayuni na Yerusalemu, atasema, “Nitamwadhibu mfalme wa Ashuru kwa ajili ya majivuno ya ukaidi wa moyo wake na kutazama kwa macho yenye dharau.”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Basi, itakuwa, Bwana atakapokuwa ameitimiza kazi yake yote juu ya mlima Sayuni na juu ya Yerusalemu, nitayaadhibu matunda ya kiburi cha moyo wake mfalme wa Ashuru, na majivuno ya macho yake.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Wakati Mwenyezi-Mungu atakapomaliza kazi zake zote mlimani Siyoni na mjini Yerusalemu, atamwadhibu mfalme wa Ashuru, kwa sababu ya majivuno na kiburi chake.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Bwana atakapokuwa amemaliza kazi yake yote dhidi ya Mlima Sayuni na Yerusalemu, atasema, “Nitamwadhibu mfalme wa Ashuru kwa ajili ya majivuno ya ukaidi wa moyo wake na kutazama kwa macho yenye dharau.”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Bwana atakapokuwa amemaliza kazi yake yote dhidi ya Mlima Sayuni na Yerusalemu, atasema, “Nitamwadhibu mfalme wa Ashuru kwa ajili ya majivuno ya ukaidi wa moyo wake na kutazama kwa macho yenye dharau.”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Basi, itakuwa, Bwana atakapokuwa ameitimiza kazi yake yote juu ya mlima Sayuni na juu ya Yerusalemu, nitamwadhibu matunda ya kiburi cha moyo wake mfalme wa Ashuru, na majivuno ya macho yake.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Wakati Mwenyezi-Mungu atakapomaliza kazi zake zote mlimani Siyoni na mjini Yerusalemu, atamwadhibu mfalme wa Ashuru, kwa sababu ya majivuno na kiburi chake.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Lakini hapo, Bwana atakapokuwa ameyamaliza matendo yale mlimani kwa Sioni namo Yerusalemu, ndipo, yatakapokuwa aliyoyasema kwamba: Nitauumbua moyo wa mfalme wa Asuri kwa ajili ya uzao wa ukuu wake na kwa ajili ya utukufu wa macho yake wa kujitukuza.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Basi, itakuwa, Bwana atakapokuwa ameitimiza kazi yake yote juu ya mlima Sayuni na juu ya Yerusalemu, nitayaadhibu matunda ya kiburi cha moyo wake mfalme wa Ashuru, na majivuno ya macho yake.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Wakati Yawe atakapomaliza kazi zake zote kwenye mulima Sayuni na katika Yerusalema, atamwazibu mufalme wa Asuria, kwa sababu ya majivuno na kiburi chake.