Isaiah 10:17 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Mungu aliye mwanga wa Israeli atakuwa kama moto, Mtakatifu wa Israeli atakuwa mwali wa moto ambao kwa siku moja utateketeza kila kitu: Miiba yake na mbigili zake pamoja.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Nuru ya Israeli itakuwa moto, Aliye Mtakatifu wao mwali wa moto; katika siku moja utaunguza na kuteketeza miiba na michongoma yake.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Na mwanga wa Israeli utakuwa ni moto, na Mtakatifu wake atakuwa mwali wa moto; nao utateketeza na kula mbigili zake na miiba yake katika siku moja.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Mungu aliye mwanga wa Israeli atakuwa kama moto, Mtakatifu wa Israeli atakuwa mwali wa moto ambao kwa siku moja utateketeza kila kitu: miiba yake na mbigili zake pamoja.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Nuru ya Israeli itakuwa moto, Aliye Mtakatifu wao mwali wa moto; katika siku moja utaunguza na kuteketeza miiba na michongoma yake.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Nuru ya Israeli itakuwa moto, Aliye Mtakatifu wao mwali wa moto; katika siku moja utaunguza na kuteketeza miiba na michongoma yake.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Na mwanga wa Israeli utakuwa ni moto, na Mtakatifu wake atakuwa muali wa moto; nao utateketeza na kula mbigili zake na miiba yake kwa siku moja.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Mungu aliye mwanga wa Israeli atakuwa kama moto, Mtakatifu wa Israeli atakuwa mwali wa moto ambao kwa siku moja utateketeza kila kitu: Miiba yake na mbigili zake pamoja.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Nao mwanga wa Isiraeli utawawia moto; nao utukufu wao utageuka kuwa kama ndimi za moto; zitayaunguza maboma yao yenye mibigili na mikunju, yateketee kwa siku moja tu.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Na mwanga wa Israeli utakuwa ni moto, na Mtakatifu wake atakuwa mwali wa moto; nao utateketeza na kula mbigili zake na miiba yake katika siku moja.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Mungu anayekuwa mwangaza wa Israeli atakuwa kama moto. Mutakatifu wa Israeli atakuwa ulimi wa moto ambao kwa siku moja utateketeza kila kitu, miiba yake na michongoma zake pamoja.