Isaiah 10:22 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Maana, hata kama sasa Waisraeli ni wengi kama mchanga wa pwani, ni wachache tu watakaorudi. Maangamizi yamepangwa yafanyike, nayo yatafanyika kwa haki tupu.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Ingawa watu wako, ee Israeli, ni wengi kama mchanga wa pwani, ni mabaki yao tu watakaorudi. Maangamizi yamekwisha amriwa, ni mengi tena ni haki.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Maana watu wako, Ee Israeli, wajapokuwa wengi kama mchanga wa pwani, ni mabaki tu watakaorudi; kuangamiza kumekusudiwa, kunakofurika kwa haki.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Maana, hata kama sasa Waisraeli ni wengi kama mchanga wa pwani, ni wachache tu watakaorudi. Maangamizi yamepangwa yafanyike, nayo yatafanyika kwa haki tupu.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Ingawa watu wako, Ee Israeli, ni wengi kama mchanga kando ya bahari, ni mabaki yao tu ndio watakaorudi. Maangamizi yamekwisha amriwa, ni mengi tena ni haki.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Ingawa watu wako, ee Israeli, ni wengi kama mchanga wa pwani, ni mabaki yao tu watakaorudi. Maangamizi yamekwisha amriwa, ni mengi tena ni haki.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Maana watu wako, Ee Israeli, wajapokuwa wengi kama mchanga wa pwani, ni mabaki tu watakaorudi; kuangamiza kumekusudiwa, kunakofurika kwa haki.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Maana, hata kama sasa Waisraeli ni wengi kama mchanga wa pwani, ni wachache tu watakaorudi. Maangamizi yamepangwa yafanyike, nayo yatafanyika kwa haki tupu.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Ijapo wawe wengi kama mchanga wa ufukoni, wao walio ukoo wako wa Isiraeli, watakaomgeukia watakuwa sao tu; wengine angamizo lao litatimizwa, liyatokeze maamuzi yake kuwa ya kweli kabisa.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Maana watu wako, Ee Israeli, wajapokuwa wengi kama mchanga wa pwani, ni mabaki tu watakaorudi; kuangamiza kumekusudiwa, kunakofurika kwa haki.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Maana, hata kama sasa Waisraeli ni wengi kama muchanga wa bahari, ni wachache tu watakaorudi. Maangamizi yamepangwa yafanyike, nayo yatafanyika kwa haki tu.