Isaiah 10:24 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Kwa hiyo, Bwana Mwenyezi-Mungu wa majeshi asema hivi: “Enyi watu wangu mnaokaa Siyoni msiwaogope Waashuru ambao wanawapiga kwa fimbo, wakiinua mikongojo yao dhidi yenu kama walivyofanya Wamisri.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Kwa hiyo, hili ndilo asemalo Mwenyezi Mungu, Mungu wa majeshi ya mbinguni: “Enyi watu wangu mnaoishi Sayuni, msiwaogope Waashuru, wanaowapiga ninyi kwa fimbo na kuinua rungu dhidi yenu, kama Misri ilivyofanya.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Kwa hiyo Bwana, Bwana wa majeshi, asema hivi, Enyi watu wangu mkaao katika Sayuni, msiogope Ashuru, ingawa akupiga kwa fimbo, na kuliinua gongo lake juu yako, kwa namna ya Kimisri.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Kwa hiyo, Bwana Mwenyezi-Mungu wa majeshi asema hivi: “Enyi watu wangu mnaokaa Siyoni msiwaogope Waashuru ambao wanawapiga kwa fimbo, wakiinua mikongojo yao dhidi yenu kama walivyofanya Wamisri.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Kwa hiyo, hili ndilo Bwana, BWANA Mwenye Nguvu Zote asemalo: “Enyi watu wangu mkaao Sayuni, msiwaogope Waashuru, wanaowapiga ninyi kwa fimbo na kuinua rungu dhidi yenu, kama Misri ilivyofanya.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Kwa hiyo, hili ndilo Bwana, bwana Mwenye Nguvu Zote asemalo: “Enyi watu wangu mkaao Sayuni, msiwaogope Waashuru, wanaowapiga ninyi kwa fimbo na kuinua rungu dhidi yenu, kama Misri ilivyofanya.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Kwa hiyo Bwana, BWANA wa majeshi, asema hivi, Enyi watu wangu mkaao katika Sayuni, msiogope Ashuru, ingawa akupiga kwa fimbo, na kuliinua gongo lake juu yako, kama walivyofanya Wamisri.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Kwa hiyo, Bwana Mwenyezi-Mungu wa majeshi asema hivi: “Enyi watu wangu mnaokaa Siyoni msiwaogope Waashuru ambao wanawapiga kwa fimbo, wakiinua mikongojo yao dhidi yenu kama walivyofanya Wamisri.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kwa hiyo Bwana Mungu Mwenye vikosi anasema hivyo: Mlio ukoo wangu ukaao Sioni, msimwogope Mwasuri, ijapo awapige vigongo, awainulie fimbo yake na kuishika njia ya Wamisri.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Kwa hiyo Bwana, BWANA wa majeshi, asema hivi, Enyi watu wangu mkaao katika Sayuni, msiogope Ashuru, ingawa akupiga kwa fimbo, na kuliinua gongo lake juu yako, kwa namna ya Kimisri.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Kwa hiyo, Bwana wetu Yawe wa majeshi anasema hivi: Enyi watu wangu munaokaa Sayuni, musiwaogope Waasuria ambao wanawapiga kwa fimbo, wakiinua gongo zao juu yenu kama walivyofanya Wamisri.