Isaiah 11:15 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Mwenyezi-Mungu atakausha ghuba ya bahari ya Shamu, kwa pumzi yake ichomayo atakausha mto Eufrate, nao utagawanyika katika vijito saba, watu wavuke humo miguu mikavu.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Mwenyezi Mungu atakausha ghuba ya bahari ya Misri; kwa upepo mkavu ataupeleka mkono wake juu ya Mto Frati. Ataugawanya katika vijito saba ili watu waweze kuuvuka wakiwa wamevaa viatu.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Na Bwana atauangamiza kabisa ulimi wa bahari ya Misri; na kwa upepo wake uteketezao atatikisa mkono wake juu ya Mto, naye ataupiga, uwe vijito saba, na kuwavusha watu wenye viatu vikavu.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Mwenyezi-Mungu atakausha ghuba ya bahari ya Shamu, kwa pumzi yake ichomayo atakausha mto Eufrate, nao utagawanyika katika vijito saba, watu wavuke humo miguu mikavu.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
BWANA atakausha ghuba ya Bahari ya Misri; kwa upepo mkavu ataupeleka mkono wake juu ya Mto Eufrati. Ataugawanya katika vijito saba ili watu waweze kuuvuka wakiwa wamevaa viatu.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
bwana atakausha ghuba ya bahari ya Misri; kwa upepo mkavu ataupeleka mkono wake juu ya Mto Frati. Ataugawanya katika vijito saba ili watu waweze kuuvuka wakiwa wamevaa viatu.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Na BWANA atauangamiza kabisa ulimi wa bahari ya Misri; na kwa upepo wake uteketezao atatikisa mkono wake juu ya Mto, naye ataupiga, uwe vijito saba, na kuwavusha watu waliovaa viatu bila kulowa.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Mwenyezi-Mungu atakausha ghuba ya bahari ya Shamu, kwa pumzi yake ichomayo atakausha mto Eufrate, nao utagawanyika katika vijito saba, watu wavuke humo miguu mikavu.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Hata ulimi wa bahari ya Misri Bwana atautia mwiko, ukauke; nalo lile jito kubwa atalikunjulia mkono wake, alifokee kwa moto wa makali yake, litokee vijito saba, watu waweze kupita pasipo kuvua viatu.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Na BWANA atauangamiza kabisa ulimi wa bahari ya Misri; na kwa upepo wake uteketezao atatikisa mkono wake juu ya Mto, naye ataupiga, uwe vijito saba, na kuwavusha watu wenye viatu vikavu.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Yawe atakausha guba ya bahari ya Misri, kwa pumzi yake inayochoma atakausha muto Furati, nao utagawanyika katika vijito saba, watu wavuke humo miguu mikavu.