Isaiah 11:6 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Mbwamwitu ataishi pamoja na mwanakondoo, chui watapumzika pamoja na mwanambuzi. Ndama na wanasimba watakula pamoja, na mtoto mdogo atawaongoza.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Mbwa-mwitu ataishi pamoja na mwana-kondoo, naye chui atalala pamoja na mbuzi, ndama, mwana simba na ng’ombe wa mwaka mmoja watakaa pamoja, naye mtoto mdogo atawaongoza.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Mbwa-mwitu atakaa pamoja na mwana-kondoo, na chui atalala pamoja na mwana-mbuzi; ndama na mwana-simba na kinono watakuwa pamoja, na mtoto mdogo atawaongoza.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Mbwamwitu ataishi pamoja na mwanakondoo, chui watapumzika pamoja na mwanambuzi. Ndama na wanasimba watakula pamoja, na mtoto mdogo atawaongoza.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Mbwa mwitu ataishi pamoja na mwana-kondoo, chui atalala pamoja na mbuzi, ndama, mwana simba na ng'ombe aliyenona wa mwaka mmoja watalisha pamoja, naye mtoto mdogo atawaongoza.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Mbwa mwitu ataishi pamoja na mwana-kondoo, naye chui atalala pamoja na mbuzi, ndama, mwana simba na ng’ombe wa mwaka mmoja watakaa pamoja, naye mtoto mdogo atawaongoza.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Mbwamwitu atakaa pamoja na mwana-kondoo, na chui atalala pamoja na mwana-mbuzi; ndama na mwanasimba na ng'ombe wanono watakuwa pamoja, na mtoto mdogo atawaongoza.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Mbwamwitu ataishi pamoja na mwanakondoo, chui watapumzika pamoja na mwanambuzi. Ndama na wanasimba watakula pamoja, na mtoto mdogo atawaongoza.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Hapo mbwa wa mwitu watafikia kwenye wana wa kondoo, nao chui watalala pamoja na wana wa mbuzi, hata ndama na simba na ng'ombe mnono watalisha pamoja, wakichungwa na mtoto mdogo.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Mbwa-mwitu atakaa pamoja na mwana-kondoo, na chui atalala pamoja na mwana-mbuzi; ndama na mwana-simba na kinono watakuwa pamoja, na mtoto mdogo atawaongoza.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Imbwa wa pori ataishi pamoja na mwana-kondoo, chui atapumzika pamoja na mwana-mbuzi. Wana-ngombe na wana-simba watakula pamoja, na mutoto mudogo atawaongoza.