Isaiah 13:16 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Watoto wao wachanga watapondwapondwa mbele yao, watanyanganywa nyumba zao, na wake zao watanajisiwa.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Watoto wao wachanga watavunjwa vipande vipande mbele ya macho yao; nyumba zao zitatekwa, na wake zao watanajisiwa.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Na watoto wao wachanga watavunjwa-vunjwa mbele ya macho yao, nyumba zao zitatekwa nyara, na wake zao watatendwa jeuri.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Watoto wao wachanga watapondwapondwa mbele yao, watanyang'anywa nyumba zao, na wake zao watanajisiwa.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Watoto wao wachanga watavunjwa vipande vipande mbele ya macho yao; nyumba zao zitatekwa na wake zao watatendwa jeuri.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Watoto wao wachanga watavunjwa vipande vipande mbele ya macho yao; nyumba zao zitatekwa na wake zao watatendwa jeuri.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Na watoto wao wachanga watavunjwavunjwa mbele ya macho yao, nyumba zao zitatekwa nyara, na wake zao watanajisiwa.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Watoto wao wachanga watapondwapondwa mbele yao, watanyanganywa nyumba zao, na wake zao watanajisiwa.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Nao watoto wao wachanga watapondwa machoni pao, nyumba zao zitatekwa, wanawake wao watatiwa soni.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Na watoto wao wachanga watavunjwa-vunjwa mbele ya macho yao, nyumba zao zitatekwa nyara, na wake zao watatendwa jeuri.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Watoto wao wachanga watapondwapondwa mbele yao, watanyanganywa nyumba zao, na watalala na wake zao kwa kinguvu.