Isaiah 13:20 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Kamwe hautakaliwa tena na watu, watu hawataishi humo katika vizazi vyote. Hakuna Mwarabu atakayepiga hema lake humo, wala mchungaji atakayechunga wanyama wake humo.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Hautakaliwa na watu kamwe, wala watu hawataishi humo kwa vizazi vyote. Hakuna Mwarabu atakayepiga hema lake huko, hakuna mchungaji atakayepumzisha makundi yake huko.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Hautakaliwa na watu tena kabisa, wala watu hawatakaa ndani yake tangu kizazi hata kizazi. Mwarabu hatapiga hema yake huko, wala wachungaji hawatalaza makundi yao huko.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Kamwe hautakaliwa tena na watu, watu hawataishi humo katika vizazi vyote. Hakuna Mwarabu atakayepiga hema lake humo, wala mchungaji atakayechunga wanyama wake humo.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Hautakaliwa na watu kamwe wala watu hawataishi humo kwa vizazi vyote, hakuna Mwarabu atakayepiga hema lake huko, hakuna mchungaji atakayepumzisha makundi yake ya kondoo na mbuzi huko.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Hautakaliwa na watu kamwe wala watu hawataishi humo kwa vizazi vyote. Hakuna Mwarabu atakayepiga hema lake huko, hakuna mchungaji atakayepumzisha makundi yake huko.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Hautakaliwa na watu tena kabisa, wala watu hawatakaa ndani yake tangu kizazi hata kizazi. Mwarabu hatapiga hema yake huko, wala wachungaji hawatalaza makundi yao huko.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Kamwe hautakaliwa tena na watu, watu hawataishi humo katika vizazi vyote. Hakuna Mwarabu atakayepiga hema lake humo, wala mchungaji atakayechunga wanyama wake humo.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Hautakaa kale na kale, wala havitatua humo vizazi na vizazi, Waarabu tu hawatapiga mle mahema yao, wala wachungaji hawatawapumzisha kondoo wao hapohapo.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Hautakaliwa na watu tena kabisa, wala watu hawatakaa ndani yake tangu kizazi hata kizazi. Mwarabu hatapiga hema yake huko, wala wachungaji hawatalaza makundi yao huko.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Hautakaliwa tena na watu hata kidogo, watu hawataishi humo katika vizazi vyote. Hakuna Mwarabu atakayesimamisha hema yake humo, wala muchungaji atakayechunga nyama wake humo.