Isaiah 13:4 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Sikilizeni kelele milimani kama za kundi kubwa la watu! Sikilizeni kelele za falme, na mataifa yanayokusanyika! Mwenyezi-Mungu wa majeshi analikagua jeshi linalokwenda vitani.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Sikilizeni kelele juu ya milima, kama ile ya umati mkubwa wa watu! Sikilizeni, makelele katika falme, kama mataifa yanayokusanyika pamoja! Mwenyezi Mungu, Mungu wa majeshi ya mbinguni anakusanya jeshi kwa ajili ya vita.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Kelele milimani kama kelele za watu wengi sana; kelele za falme za mataifa waliokutana pamoja; Bwana wa majeshi anapanga jeshi kwa vita;
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Sikilizeni kelele milimani kama za kundi kubwa la watu! Sikilizeni kelele za falme, na mataifa yanayokusanyika! Mwenyezi-Mungu wa majeshi analikagua jeshi linalokwenda vitani.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Sikilizeni kelele juu ya milima, kama ile ya umati mkubwa wa watu! Sikilizeni, makelele katikati ya falme, kama mataifa yanayokusanyika pamoja! BWANA Mwenye Nguvu Zote anakusanya jeshi kwa ajili ya vita.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Sikilizeni kelele juu ya milima, kama ile ya umati mkubwa wa watu! Sikilizeni, makelele katikati ya falme, kama mataifa yanayokusanyika pamoja! bwana Mwenye Nguvu Zote anakusanya jeshi kwa ajili ya vita.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Kelele milimani kama kelele za watu wengi sana; kelele za falme za mataifa waliokutana pamoja; BWANA wa majeshi anapanga jeshi kwa vita;
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Sikilizeni kelele milimani kama za kundi kubwa la watu! Sikilizeni kelele za falme, na mataifa yanayokusanyika! Mwenyezi-Mungu wa majeshi analikagua jeshi linalokwenda vitani.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Makelele mengi mno yako milimani kama ni ya watu wengi, sauti za uvumi ziko za wafalme wanaokusanya watu wao. Bwana Mwenye vikosi anavitazama vikosi vyake vya kwenda vitani.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Kelele milimani kama kelele za watu wengi sana; kelele za falme za mataifa waliokutana pamoja; BWANA wa majeshi anapanga jeshi kwa vita;
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Musikilize kelele kwenye milima kama za kundi kubwa la watu! Musikilize kelele za falme, na mataifa yanayokusanyika! Yawe wa majeshi analichunguza kundi linalokwenda kwa vita.