Isaiah 13:8 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Watu watafadhaika, watashikwa na hofu na maumivu, watakuwa na uchungu kama mama anayejifungua. Watatazamana kwa mashaka, nyuso zao zitawaiva kwa haya.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Hofu itawakamata, uchungu na maumivu makali yatawashika, watagaagaa kama mwanamke aliye na uchungu wa kuzaa. Watatazamana kwa hofu kila mtu na mwenzake, nyuso zao zikiwaka kama moto.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Nao watafadhaika; watashikwa na utungu na maumivu; watakuwa na utungu kama mwanamke aliye karibu na kuzaa; watakodoleana macho; nyuso zao zitakuwa ni nyuso za moto.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Watu watafadhaika, watashikwa na hofu na maumivu, watakuwa na uchungu kama mama anayejifungua. Watatazamana kwa mashaka, nyuso zao zitawaiva kwa haya.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Hofu itawakamata, uchungu na maumivu makali yatawashika, watajinyonganyonga kama mwanamke aliye na utungu wa kuzaa. Watatazamana kwa hofu kila mtu na mwenzake, nyuso zao zikiwa katika hali ya kuwaka kama moto.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Hofu itawakamata, uchungu na maumivu makali yatawashika, watagaagaa kama mwanamke aliye na utungu wa kuzaa. Watatazamana kwa hofu kila mtu na mwenzake, nyuso zao zikiwaka kama moto.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Nao watafadhaika; watashikwa na uchungu na maumivu; watakuwa na uchungu kama mwanamke aliye karibu kuzaa; watakodoleana macho; nyuso zao zitakuwa ni nyuso za moto.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Watu watafadhaika, watashikwa na hofu na maumivu, watakuwa na uchungu kama mama anayejifungua. Watatazamana kwa mashaka, nyuso zao zitawaiva kwa haya.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Vituko na masongano na maumivu yatawashika, wajipinde kama mzazi, watatumbulizana macho kwa kushangaa, nyuso zao zitawaiva kama ni zenye moto.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Nao watafadhaika; watashikwa na utungu na maumivu; watakuwa na utungu kama mwanamke aliye karibu na kuzaa; watakodoleana macho; nyuso zao zitakuwa ni nyuso za moto.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Watu watafazaika, watashikwa na hofu na maumivu, watakuwa na uchungu kama mama anapozaa. Wataangalia kwa mashaka, nyuso zao zitaungua kwa haya.