Isaiah 13:9 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Siku ya Mwenyezi-Mungu inakuja, siku kali, ya ghadhabu na hasira kali. Itaifanya nchi kuwa uharibifu, itawaangamiza wenye dhambi wake.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Tazameni, siku ya Mwenyezi Mungu inakuja, siku katili, yenye ghadhabu na hasira kali, kuifanya nchi kuwa ukiwa, na kuwaangamiza wenye dhambi waliomo.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Tazama, siku ya Bwana inakuja, siku kali, ya hasira na ghadhabu kuu, ili iifanye nchi kuwa ukiwa, na kuwaharibu watu wake, wenye dhambi, wasikae ndani yake.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Siku ya Mwenyezi-Mungu inakuja, siku kali, ya ghadhabu na hasira kali. Itaifanya nchi kuwa uharibifu, itawaangamiza wenye dhambi wake.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Tazameni, siku ya BWANA inakuja, siku katili, yenye ghadhabu na hasira kali, kuifanya nchi kuwa ukiwa na kuwaangamiza wenye dhambi waliomo ndani yake.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Tazameni, siku ya bwana inakuja, siku katili, yenye ghadhabu na hasira kali, kuifanya nchi kuwa ukiwa na kuwaangamiza wenye dhambi waliomo ndani yake.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Tazama, siku ya BWANA inakuja, siku kali, ya hasira na ghadhabu kuu, ili iifanye nchi kuwa ukiwa, na kuwaharibu watu wake, wenye dhambi, wasikae ndani yake.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Siku ya Mwenyezi-Mungu inakuja, siku kali, ya ghadhabu na hasira kali. Itaifanya nchi kuwa uharibifu, itawaangamiza wenye dhambi wake.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Tazameni: Siku ya Bwana inakuja, inaleta mastuko na makali na machafuko yenye moto, yaziangamize nchi, ziwe jangwa, kwa kuwamaliza wakosaji, wasikae.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Tazama, siku ya BWANA inakuja, siku kali, ya hasira na ghadhabu kuu, ili iifanye nchi kuwa ukiwa, na kuwaharibu watu wake, wenye dhambi, wasikae ndani yake.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Siku ya Yawe inakuja, siku kali, ya kasirani na hasira kali. Itaifanya inchi kuwa uharibifu, itawaangamiza wenye zambi ndani yake.