Isaiah 14:2 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Watu wa mataifa watawasaidia Waisraeli kurudi katika nchi waliyopewa na Mwenyezi-Mungu. Na hapo watawatumikia Waisraeli kama watumwa. Wale waliowateka sasa watatekwa na Waisraeli, na watawatawala wale waliowadhulumu.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Mataifa watawachukua na kuwaleta mahali pao wenyewe. Nayo nyumba ya Israeli itamiliki mataifa kama watumishi na wajakazi katika nchi ya Mwenyezi Mungu. Watawafanya watekaji wao kuwa mateka, na kuwatawala waliowadhulumu.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Na hao mataifa watawatwaa na kuwaleta mpaka mahali pao wenyewe, na nyumba ya Israeli watawamiliki, na kuwafanya watumishi na wajakazi katika nchi ya Bwana; nao watawachukua hali ya kufungwa watu wale waliowafunga wao, nao watawamiliki watu wale waliowaonea.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Watu wa mataifa watawasaidia Waisraeli kurudi katika nchi waliyopewa na Mwenyezi-Mungu. Na hapo watawatumikia Waisraeli kama watumwa. Wale waliowateka sasa watatekwa na Waisraeli, na watawatawala wale waliowadhulumu.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Mataifa watawachukua na kuwaleta mahali pao wenyewe. Nayo nyumba ya Israeli itamiliki mataifa kama watumishi wa kiume na watumishi wa kike katika nchi ya BWANA. Watawafanya watekaji wao kuwa mateka na kutawala juu ya wale waliowaonea.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Mataifa watawachukua na kuwaleta mahali pao wenyewe. Nayo nyumba ya Israeli itamiliki mataifa kama watumishi na wajakazi katika nchi ya bwana. Watawafanya watekaji wao kuwa mateka, na kutawala juu ya wale waliowaonea.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Na hao mataifa watawatwaa na kuwaleta mpaka mahali pao wenyewe, na nyumba ya Israeli watawamiliki, na kuwafanya watumishi na wajakazi katika nchi ya BWANA; nao watawachukua hali ya kufungwa watu wale waliowafunga wao, nao watawamiliki watu wale waliowaonea.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Watu wa mataifa watawasaidia Waisraeli kurudi katika nchi waliyopewa na Mwenyezi-Mungu. Na hapo watawatumikia Waisraeli kama watumwa. Wale waliowateka sasa watatekwa na Waisraeli, na watawatawala wale waliowadhulumu.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Watu wengine watawachukua, wawapeleke kwao, kisha mlango wa Isiraeli utawatumia katika nchi ya Bwana kuwa watumishi wao wa kiume na wa kike. Hivyo watawateka waliowateka, wawatawale waliowasonga.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Na hao mataifa watawatwaa na kuwaleta mpaka mahali pao wenyewe, na nyumba ya Israeli watawamiliki, na kuwafanya watumishi na wajakazi katika nchi ya BWANA; nao watawachukua hali ya kufungwa watu wale waliowafunga wao, nao watawamiliki watu wale waliowaonea.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Watu wa mataifa watawasaidia Waisraeli kurudi katika inchi waliyopewa na Yawe. Na hapo watawatumikia Waisraeli kama watumwa. Wale waliowateka sasa watatekwa na Waisraeli, na watawatawala wale waliowatesa.