Isaiah 14:23 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Nitaufanya kuwa makao ya nungunungu, na utakuwa madimbwi ya maji. Nami nitaufagilia mbali kwa ufagio wa maangamizi. Mimi Mwenyezi-Mungu wa majeshi nimenena.”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
“Nitaifanya kuwa mahali pa bundi, na kuwa nchi ya matope; nitaifagia kwa ufagio wa maangamizi,” asema Mwenyezi Mungu, Mungu wa majeshi ya mbinguni.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Tena nitaifanya hiyo nchi kuwa makao ya nungu, na maziwa ya maji; nami nitaifagilia mbali kwa ufagio wa uharibifu; asema Bwana wa majeshi.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Nitaufanya kuwa makao ya nungunungu, na utakuwa madimbwi ya maji. Nami nitaufagilia mbali kwa ufagio wa maangamizi. Mimi Mwenyezi-Mungu wa majeshi nimenena.”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
“Nitaifanya kuwa mahali pa bundi, na kuwa nchi ya matope; nitaifagia kwa ufagio wa maangamizi,” asema BWANA Mwenye Nguvu Zote.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
“Nitaifanya kuwa mahali pa bundi, na kuwa nchi ya matope; nitaifagia kwa ufagio wa maangamizi,” asema bwana Mwenye Nguvu Zote.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Tena nitaifanya hiyo nchi kuwa makao ya nungunungu, na maziwa ya maji; nami nitaifagilia mbali kwa ufagio wa uharibifu; asema BWANA wa majeshi.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Nitaufanya kuwa makao ya nungunungu, na utakuwa madimbwi ya maji. Nami nitaufagilia mbali kwa ufagio wa maangamizi. Mimi Mwenyezi-Mungu wa majeshi nimenena.”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Nitaiweka nchi yao kuwa kao lao nungu, iwe yenye mabwawa ya matopetope tu; nitapazoa kabisa na kutumia kizoleo kiangamizacho! Ndivyo, asemavyo Bwana Mwenye vikosi.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Tena nitaifanya hiyo nchi kuwa makao ya nungu, na maziwa ya maji; nami nitaifagilia mbali kwa ufagio wa uharibifu; asema BWANA wa majeshi.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Nitaufanya kuwa makao ya nungunungu, na utakuwa tingitingi ya maji. Nami nitaufagilia mbali kwa ufagio wa maangamizi. –Ni ujumbe wa Yawe wa majeshi.