Isaiah 14:9 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
“Kuzimu nako kumechangamka, ili kukulaki wakati utakapokuja. Kunaiamsha mizimu ije kukusalimu na wote waliokuwa wakuu wa dunia; huwaamsha kutoka viti vyao vya enzi wote waliokuwa wafalme wa mataifa.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Kuzimu kumetaharuki kukulaki unapokuja, kunaamsha roho za waliokufa ili kukupokea, wote waliokuwa viongozi katika ulimwengu, kunawafanya wainuke kwenye viti vyao vya kifalme: wale wote waliokuwa wafalme juu ya mataifa.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Kuzimu chini kumetaharuki kwa ajili yako, Ili kukulaki utakapokuja; Huwaamsha waliokufa kwa ajili yako, Naam, walio wakuu wote wa dunia; Huwainua wafalme wote wa mataifa, Watoke katika viti vyao vya enzi.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
“Kuzimu nako kumechangamka, ili kukulaki wakati utakapokuja. Kunaiamsha mizimu ije kukusalimu na wote waliokuwa wakuu wa dunia; huwaamsha kutoka viti vyao vya enzi wote waliokuwa wafalme wa mataifa.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Huko chini Kuzimu kote kumetaharuki kukulaki unapokuja, inaamsha roho za waliokufa ili kukupokea, wote waliokuwa viongozi katika ulimwengu, inawafanya wainuke kwenye viti vyao vya kifalme, wale wote waliokuwa wafalme juu ya mataifa.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Kuzimu kote kumetaharuki kukulaki unapokuja, kunaamsha roho za waliokufa ili kukupokea, wote waliokuwa viongozi katika ulimwengu, kunawafanya wainuke kwenye viti vyao vya kifalme: wale wote waliokuwa wafalme juu ya mataifa.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Kuzimu chini kumetaharuki kwa ajili yako, Ili kukulaki utakapokuja; Huwaamsha waliokufa kwa ajili yako, Naam, walio wakuu wote wa dunia; Huwainua wafalme wote wa mataifa, Watoke katika viti vyao vya enzi.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
“Kuzimu nako kumechangamka, ili kukulaki wakati utakapokuja. Kunaiamsha mizimu ije kukusalimu na wote waliokuwa wakuu wa dunia; huwaamsha kutoka viti vyao vya enzi wote waliokuwa wafalme wa mataifa.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kule chini kuzimuni kumevurugika kwa ajili yako: kwa kungoja, uje, kukawaamsha wazimu wote, waliokuwa wenye nguvu katika nchi, kukawainua wafalme wote, wao wa kimizimu, waondoke katika viti vyao vilivyo vya kifalme.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Kuzimu chini kumetaharuki kwa ajili yako, Ili kukulaki utakapokuja; Huwaamsha waliokufa kwa ajili yako, Naam, walio wakuu wote wa dunia; Huwainua wafalme wote wa mataifa, Watoke katika viti vyao vya enzi.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Kuzimu nako kumechangamuka, kusudi ya kukupokea wakati utakapokuja. Kunaiamusha mizimu ikuje kukusalimia na wote waliokuwa wakubwa wa dunia; kunawasimamisha kutoka kwenye viti vyao vya kifalme wote waliokuwa wafalme wa mataifa.