Isaiah 15:2 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Watu wa Diboni wamepanda hekaluni, hadi mahali pa juu kuomboleza, watu wa Moabu wanalia kwa ajili ya Nebo na Medeba; vichwa vyote vimenyolewa upara, ndevu zao zote zimekatwa kabisa.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Diboni anakwea hadi kwenye hekalu lake, hadi mahali pake pa juu pa kuabudia ili walie, Moabu anaombolezea Nebo na Medeba. Kila kichwa kimenyolewa na kila ndevu limeondolewa.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Wanapanda juu hata Bayithi na Diboni, mpaka mahali palipo juu ili walie; juu ya Nebo na juu ya Medeba Wamoabi wanalia; Wana upaa juu ya vichwa vyao vyote; kila ndevu zimenyolewa.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Watu wa Diboni wamepanda hekaluni, hadi mahali pa juu kuomboleza, watu wa Moabu wanalia kwa ajili ya Nebo na Medeba; vichwa vyote vimenyolewa upara, ndevu zao zote zimekatwa kabisa.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Diboni anakwea hadi kwenye Hekalu lake, mpaka mahali pake pa juu pa kuabudia miungu ili walie, Moabu anaombolezea Nebo na Medeba. Kila kichwa kimenyolewa na kila ndevu zimeondolewa.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Diboni anakwea hadi kwenye hekalu lake, mpaka mahali pake pa juu ili walie, Moabu anaombolezea Nebo na Medeba. Kila kichwa kimenyolewa na kila ndevu limeondolewa.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Wanapanda juu hata Bayithi na Diboni, mpaka mahali palipo juu ili walie; juu ya Nebo na juu ya Medeba Wamoabi wanalia; wana upaa juu ya vichwa vyao vyote; kila ndevu zimenyolewa.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Watu wa Diboni wamepanda hekaluni, hadi mahali pa juu kuomboleza, watu wa Moabu wanalia kwa ajili ya Nebo na Medeba; vichwa vyote vimenyolewa upara, ndevu zao zote zimekatwa kabisa.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Wabeti na Wadiboni wanapanda vilimani kupiga vilio; kule Nebo na Medeba Wamoabu wanaomboleza, vichwa vyao vyote viko na vipara, nazo ndevu zote zimekatwa.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Wanapanda juu hata Bayithi na Diboni, mpaka mahali palipo juu ili walie; juu ya Nebo na juu ya Medeba Wamoabi wanalia; Wana upaa juu ya vichwa vyao vyote; kila ndevu zimenyolewa.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Watu wa Diboni wamepanda katika hekalu pahali pa juu kwa kuomboleza, watu wa Moabu wanalia kwa ajili ya Nebo na Medeba; vichwa vyote vimenyolewa upaa, ndevu zao zote zimekatwa kabisa.