Isaiah 15:3 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Wanapita njiani wamevaa mavazi ya gunia. Kwenye paa za nyumba na viwanja vya mji watu wanalia na kukauka kwa machozi.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Wamevaa magunia barabarani; juu ya mapaa na kwenye viwanja wote wanaomboleza, wakilala kifudifudi na kulia.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Wanajivika nguo za magunia katika njia kuu zao; juu ya dari zao, na katika mitaa yao, kila mtu analia, anamwaga machozi.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Wanapita njiani wamevaa mavazi ya gunia. Kwenye paa za nyumba na viwanja vya mji watu wanalia na kukauka kwa machozi.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Wamevaa nguo za magunia barabarani, juu ya mapaa na kwenye viwanja wote wanaomboleza, hulala kifudifudi kwa kulia.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Wamevaa nguo za magunia barabarani, juu ya mapaa na kwenye viwanja wote wanaomboleza, wamelala kifudifudi kwa kulia.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Wanajivika nguo za magunia katika njia kuu zao; juu ya madari yao, na katika mitaa yao, kila mtu analia, anamwaga machozi.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Wanapita njiani wamevaa mavazi ya gunia. Kwenye paa za nyumba na viwanja vya mji watu wanalia na kukauka kwa machozi.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Wakitoka nje huwa wamejivika magunia, wao wote, kama wamo vipaani au kama wamo mawanjani, wanapiga vilio na kutoa machozi.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Wanajivika nguo za magunia katika njia kuu zao; juu ya dari zao, na katika mitaa yao, kila mtu analia, anamwaga machozi.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Wanapita katika njia wakivaa magunia. Kwenye paa za nyumba na viwanja vya muji watu wanalia na kukauka kwa machozi.