Isaiah 15:5 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Moyo wangu unasononeka juu ya nchi ya Moabu; wakimbizi wake wanakimbilia Soari, wanakimbia mpaka Eglath-shelishiya. Wanapanda njia ya kwenda Luhithi wakilia, njiani kwenda Horonaimu wanatoa kilio cha maangamizi.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Moyo wangu unamlilia Moabu; wakimbizi wake wanakimbilia Soari, hadi Eglath-Shelishiya. Wanapanda njia ya kwenda Luhithi, wanaenda huku wanalia; barabarani iendayo Horonaimu wanaombolezea maangamizi yao.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Moyo wangu unamlilia Moabu; wakuu wake wanakimbilia Soari kama ndama wa miaka mitatu; kwa maana wanapanda mbavu za Luhithi wakilia; maana katika njia iendayo hata Horonaimu wanapaliza sauti ya kukata tamaa.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Moyo wangu unasononeka juu ya nchi ya Moabu; wakimbizi wake wanakimbilia Soari, wanakimbia mpaka Eglath-shelishiya. Wanapanda njia ya kwenda Luhithi wakilia, njiani kwenda Horonaimu wanatoa kilio cha maangamizi.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Moyo wangu unamlilia Moabu; wakimbizi wake wanakimbilia Soari, hadi Eglath-Shelishiya. Wanapanda njia ya kwenda Luhithi, wanakwenda huku wanalia; kwenye barabara iendayo Horonaimu wanaombolezea maangamizi yao.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Moyo wangu unamlilia Moabu; wakimbizi wake wanakimbilia Soari, hadi Eglath-Shelishiya. Wanapanda njia ya kwenda Luhithi, wanakwenda huku wanalia; barabarani iendayo Horonaimu wanaombolezea maangamizi yao.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Moyo wangu unamlilia Moabu; wakuu wake wanakimbilia Soari kama ndama wa miaka mitatu; kwa maana wanapanda mbavu za Luhithi wakilia; maana katika njia iendayo hata Horonaimu wanatoa kilio cha maangamizi.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Moyo wangu unasononeka juu ya nchi ya Moabu; wakimbizi wake wanakimbilia Soari, wanakimbia mpaka Eglath-shelishiya. Wanapanda njia ya kwenda Luhithi wakilia, njiani kwenda Horonaimu wanatoa kilio cha maangamizi.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Moyo wangu unawalilia Wamoabu, kwa kukimbizwa wamefika Soari na Eglati wa tatu, hata njia za Luhiti watu wanazipanda na kulia, vilevile njiani kwenda Horonemu wanapiga makelele ya kuyalilia maangamizo.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Moyo wangu unamlilia Moabu; wakuu wake wanakimbilia Soari kama ndama wa miaka mitatu; kwa maana wanapanda mbavu za Luhithi wakilia; maana katika njia iendayo hata Horonaimu wanapaliza sauti ya kukata tamaa.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Moyo wangu unaugua kwa ajili ya inchi ya Moabu; wakimbizi wake wanakimbilia Zoari, wanakimbia mpaka Egilati-Selisiya. Wanapanda njia ya kwenda Luhiti wakilia, katika njia kwenda Horonaimu wanatoa kilio cha maangamizi.