Isaiah 16:10 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Furaha na shangwe zimetoweka katika shamba la rutuba. Kwenye mizabibu hakuna kuimba tena, wala kupiga vigelegele. Hakuna tena kukamua zabibu shinikizoni, sauti za furaha za mavuno zimekomeshwa.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Furaha na shangwe zimeondolewa kutoka mashamba ya matunda; hakuna yeyote aimbaye wala apazaye sauti katika mashamba ya mizabibu; hakuna yeyote akanyagaye zabibu shinikizoni, kwa kuwa nimekomesha makelele.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Na furaha imeondolewa, na shangwe toka mashamba yaliyozaa sana; hapana kuimba katika mashamba ya mizabibu, wala sauti za furaha; akanyagaye hakanyagi divai katika mashinikizo; nimeikomesha sauti ya furaha yake akanyagaye.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Furaha na shangwe zimetoweka katika shamba la rutuba. Kwenye mizabibu hakuna kuimba tena, wala kupiga vigelegele. Hakuna tena kukamua zabibu shinikizoni, sauti za furaha za mavuno zimekomeshwa.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Furaha na shangwe zimeondolewa kutoka katika mashamba ya matunda; hakuna ye yote aimbaye wala apazaye sauti katika mashamba ya mizabibu; hakuna ye yote akanyagaye zabibu shinikizoni, kwa kuwa nimekomesha makelele.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Furaha na shangwe zimeondolewa kutoka mashamba ya matunda; hakuna yeyote aimbaye wala apazaye sauti katika mashamba ya mizabibu; hakuna yeyote akanyagaye zabibu shinikizoni, kwa kuwa nimekomesha makelele.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Na furaha imeondolewa, na shangwe toka mashamba yaliyozaa sana; hapana kuimba katika mashamba ya mizabibu, wala sauti za furaha; akanyagaye hakanyagi divai katika mashinikizo; nimeikomesha sauti ya furaha yake akanyagaye.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Furaha na shangwe zimetoweka katika shamba la rutuba. Kwenye mizabibu hakuna kuimba tena, wala kupiga vigelegele. Hakuna tena kukamua zabibu shinikizoni, sauti za furaha za mavuno zimekomeshwa.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Shangwe za furaha zikatoweka mashambani, nako mizabibuni hawapigi vigelegele wala mashangilio, wala hakuna anayekamulia mvinyo makamulioni, nyimbo za wakamuliaji nimezinyamazisha.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Na furaha imeondolewa, na shangwe toka mashamba yaliyozaa sana; hapana kuimba katika mashamba ya mizabibu, wala sauti za furaha; akanyagaye hakanyagi divai katika mashinikizo; nimeikomesha sauti ya furaha yake akanyagaye.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Furaha na shangwe zimetoweka katika shamba lenyi mavuno mengi. Kwenye mizabibu hakuna kuimba tena, wala kupiga vigelegele. Hakuna tena kukamua zabibu ndani ya vikamulio, sauti za furaha za mavuno zimekomeshwa.