Isaiah 16:12 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Watu wa Moabu wanapojitokeza kuabudu mungu wao, wanapojichosha huko juu mahali pa ibada, wanapokwenda mahali pao patakatifu kusali, hawatakubaliwa.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Moabu anapojitokeza mahali pake pa juu pa kuabudia, anajichosha mwenyewe tu; anapoenda mahali pake pa ibada za sanamu ili kuomba, haitamfaidi lolote.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Tena itakuwa, Moabu akionekana, na kujichosha kwa kulia juu ya mahali pa juu, na kuingia katika patakatifu pake aombe, hatapata kushinda.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Watu wa Moabu wanapojitokeza kuabudu mungu wao, wanapojichosha huko juu mahali pa ibada, wanapokwenda mahali pao patakatifu kusali, hawatakubaliwa.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Wakati Moabu anapojitokeza mahali pake pa juu, anajichosha mwenyewe tu; anapokwenda mahali pake pa kuabudia miungu ili kuomba, haitamfaidia lo lote.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Wakati Moabu anapojitokeza mahali pake pa juu, anajichosha mwenyewe tu; anapokwenda mahali pake pa kuabudia miungu ili kuomba, haitamfaidi lolote.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Tena itakuwa, Moabu akionekana, na kujichosha kwa kulia juu ya mahali pa juu, na kuingia katika patakatifu pake aombe, hatapata kushinda.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Watu wa Moabu wanapojitokeza kuabudu mungu wao, wanapojichosha huko juu mahali pa ibada, wanapokwenda mahali pao patakatifu kusali, hawatakubaliwa.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Napo hapo, Wamoabu watakapotokea vilimani juu na kujisumbulia hapohapo, napo, watakapoingia patakatifu pao kuomba, hakuna watakachojipatia.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Tena itakuwa, Moabu akionekana, na kujichosha kwa kulia juu ya mahali pa juu, na kuingia katika patakatifu pake aombe, hatapata kushinda.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Watu wa Moabu wanapojitokeza kuabudu mungu wao, wanapojichokesha huko juu pahali pa ibada, wanapokwenda pahali pao patakatifu kwa kuomba, hawatakubaliwa.