Isaiah 16:14 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Lakini sasa Mwenyezi-Mungu asema hivi: “Baada ya miaka mitatu kamili, ikihesabiwa kama mfanyakazi anavyohesabu siku zake, fahari ya Moabu itakwisha. Ingawa watu wake ni wengi, watakaobaki hai watakuwa wachache na wanyonge.”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Lakini sasa Mwenyezi Mungu anasema: “Katika miaka mitatu, kama vile mtumishi aliyefungwa na mkataba angeihesabu, fahari ya Moabu na watu wake wengi watadharauliwa, nao walionusurika watakuwa wachache sana, tena wanyonge.”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Lakini sasa Bwana asema hivi, Katika muda wa miaka mitatu, kama miaka ya mtu wa mshahara, utukufu wa Moabu utadharauliwa, pamoja na wingi wake wote; mabaki yake yatakuwa machache sana, kama si kitu kabisa.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Lakini sasa Mwenyezi-Mungu asema hivi: “Baada ya miaka mitatu kamili, ikihesabiwa kama mfanyakazi anavyohesabu siku zake, fahari ya Moabu itakwisha. Ingawa watu wake ni wengi, watakaobaki hai watakuwa wachache na wanyonge.”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Lakini sasa BWANA anasema: “Katika miaka mitatu, kama vile mtumishi aliyefungwa na mkataba angeihesabu, fahari ya Moabu na watu wake wengi watadharauliwa, nao walionusurika watakuwa wachache sana tena wanyonge.”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Lakini sasa bwana anasema: “Katika miaka mitatu, kama vile mtumishi aliyefungwa na mkataba angeihesabu, fahari ya Moabu na watu wake wengi watadharauliwa, nao walionusurika watakuwa wachache sana, tena wanyonge.”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Lakini sasa BWANA asema hivi, Katika muda wa miaka mitatu, kama miaka ya mtu wa mshahara, utukufu wa Moabu utadharauliwa, licha ya wingi wa watu wake; na watakaobaki watakuwa wachache sana na dhaifu.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Lakini sasa Mwenyezi-Mungu asema hivi: “Baada ya miaka mitatu kamili, ikihesabiwa kama mfanyakazi anavyohesabu siku zake, fahari ya Moabu itakwisha. Ingawa watu wake ni wengi, watakaobaki hai watakuwa wachache na wanyonge.”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
lakini sasa Bwana anasema hivi: Itakapotimia miaka mitatu iliyo kama miaka ya kibarua, ndipo, utukufu wa Moabu utakapokuwa umebezeka, nao ulikuwa haukupimika kwa wingi wa watu, nalo sao lao litakuwa limepunguka, liwe dogo sana pasipo nguvu zo zote.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Lakini sasa BWANA asema hivi, Katika muda wa miaka mitatu, kama miaka ya mtu wa mshahara, utukufu wa Moabu utadharauliwa, pamoja na wingi wake wote; mabaki yake yatakuwa machache sana, kama si kitu kabisa.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Lakini sasa Yawe anasema hivi: Nyuma ya miaka mitatu kamili, ikihesabiwa kama vile mutumishi anavyohesabu siku zake, utukufu wa Moabu utapunguka. Ingawa watu wake ni wengi, watakaobaki wazima watakuwa wachache na wazaifu.