Isaiah 16:2 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Kama ndege wanavyohangaika na kurukaruka, wakiwa wamefukuzwa kutoka viota vyao, ndivyo walivyo mabinti wa Moabu kwenye vivuko vya Arnoni.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Kama ndege wanaopapatika waliofukuzwa kutoka kiota, ndivyo walivyo wanawake wa Moabu kwenye vivuko vya Mto Arnoni.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Na binti za Moabu watakuwa kama ndege warukao huko na huko, kama kioto cha ndege waliotiwa hofu, kwenye vivuko vya Arnoni.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Kama ndege wanavyohangaika na kurukaruka, wakiwa wamefukuzwa kutoka viota vyao, ndivyo walivyo mabinti wa Moabu kwenye vivuko vya Arnoni.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Kama ndege wanaopapatika waliofukuzwa kutoka kwenye kiota chao, ndivyo walivyo wanawake wa Moabu kwenye vivuko vya Arnoni.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Kama ndege wanaopapatika waliofukuzwa kutoka kwenye kiota, ndivyo walivyo wanawake wa Moabu kwenye vivuko vya Arnoni.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Na binti za Moabu watakuwa kama ndege warukao huku na huko, kama kiota cha ndege waliotiwa hofu, kwenye vivuko vya Arnoni.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Kama ndege wanavyohangaika na kurukaruka, wakiwa wamefukuzwa kutoka viota vyao, ndivyo walivyo mabinti wa Moabu kwenye vivuko vya Arnoni.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kama ndege wanavyohangaika na kurukaruka wakistushwa matunduni mwao, ndivyo, wana wa Moabu watakavyokuwa na kuvikimbilia vivuko vya Arnoni.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Na binti za Moabu watakuwa kama ndege warukao huko na huko, kama kioto cha ndege waliotiwa hofu, kwenye vivuko vya Arnoni.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Kama ndege wanavyohangaika na kurukaruka, wakiwa wamefukuzwa kutoka chicha zao, ndivyo wabinti wa Moabu wanavyokuwa kwenye vivuko vya Arnoni.