Isaiah 16:5 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
utawala adili utazinduliwa katika maskani ya Daudi, mtawala apendaye kutenda haki, na mwepesi wa kufanya yaliyo sawa; atatawala humo kwa uaminifu.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Kwa upendo kiti cha utawala kitaimarishwa, kwa uaminifu mtu ataketi juu yake, yeye atokaye nyumba ya Daudi: yeye ambaye katika kuhukumu hutafuta haki, na huhimiza njia ya haki.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Na kiti cha enzi kitafanywa imara kwa rehema; na mmoja ataketi juu yake katika kweli, katika hema ya Daudi; akifanya hukumu, akitaka sana yaliyo haki, mwepesi wa kutenda haki.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
utawala adili utazinduliwa katika maskani ya Daudi, mtawala apendaye kutenda haki, na mwepesi wa kufanya yaliyo sawa; atatawala humo kwa uaminifu.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Kwa upendo kiti cha enzi kitaimarishwa, kwa uaminifu mtu ataketi juu yake, yeye atokaye katika nyumba ya Daudi: yeye ambaye katika kuhukumu hutafuta haki, na huhimiza njia ya haki.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Kwa upendo kiti cha enzi kitaimarishwa, kwa uaminifu mtu ataketi juu yake, yeye atokaye nyumba ya Daudi: yeye ambaye katika kuhukumu hutafuta haki, na huhimiza njia ya haki.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Na kiti cha enzi kitafanywa imara kwa rehema; na mmoja ataketi juu yake katika kweli, katika hema ya Daudi; akifanya hukumu, akitaka sana yaliyo haki, mwepesi wa kutenda haki.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
utawala adili utazinduliwa katika maskani ya Daudi, mtawala apendaye kutenda haki, na mwepesi wa kufanya yaliyo sawa; atatawala humo kwa uaminifu.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Hapo kiti cha kifalme kitasimikwa kwa upole, naye atakayekikalia kwa welekevu hemani mwa Dawidi atakuwa mwamuzi atafutaye yanyokayo kwa kujua wongofu.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Na kiti cha enzi kitafanywa imara kwa rehema; na mmoja ataketi juu yake katika kweli, katika hema ya Daudi; akifanya hukumu, akitaka sana yaliyo haki, mwepesi wa kutenda haki.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Kisha utawala wa wema utazinduliwa katika hema ya Daudi. Mutawala atakuwa mwaminifu. Atahukumu kufuatana na sheria ya Mungu, atakuwa mwepesi wa kutenda kwa haki.