Isaiah 16:8 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Mashamba ya Heshboni yamefifia. Kadhalika na zabibu za Sibma ambazo ziliwalevya wakuu wa mataifa zikafika Yazeri na kusambaa hata jangwani, chipukizi zake zikafika hata ngambo ya bahari.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Mashamba ya Heshboni yananyauka, pia na mizabibu ya Sibma. Watawala wa mataifa wamekanyaga mizabibu iliyo mizuri sana, ambayo ilipata kufika Yazeri na kuenea kuelekea jangwani. Machipukizi yake yalienea yakafika hadi baharini.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Maana makonde ya Heshboni yamenyauka, na mzabibu wa Sibma; mabwana wa mataifa wameyavunja matawi yake mateule; yamefika hata Yazeri, yalitanga-tanga hata nyikani; matawi yake yalitapakaa, yaliivuka bahari.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Mashamba ya Heshboni yamefifia. Kadhalika na zabibu za Sibma ambazo ziliwalevya wakuu wa mataifa zikafika Yazeri na kusambaa hata jangwani, chipukizi zake zikafika hata ng'ambo ya bahari.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Mashamba ya Heshboni yananyauka, pia na mizabibu ya Sibma. Watawala wa mataifa wamekanyaga mizabibu iliyo mizuri sana, ambayo ilipata kufika Yazeri na kuenea kuelekea jangwani. Machipukizi yake yalienea yakafika hadi baharini.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Mashamba ya Heshboni yananyauka, pia na mizabibu ya Sibma. Watawala wa mataifa wamekanyaga mizabibu iliyo mizuri sana, ambayo ilipata kufika Yazeri na kuenea kuelekea jangwani. Machipukizi yake yalienea yakafika hadi baharini.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Maana mashamba ya Heshboni yamenyauka, na mzabibu wa Sibma; mabwana wa mataifa wameyavunja matawi yake mateule; yamefika hadi Yazeri, yalitangatanga hadi jangwani matawi yake yalitapakaa, yaliivuka bahari.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Mashamba ya Heshboni yamefifia. Kadhalika na zabibu za Sibma ambazo ziliwalevya wakuu wa mataifa zikafika Yazeri na kusambaa hata jangwani, chipukizi zake zikafika hata ngambo ya bahari.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kwani mashamba ya Hesiboni yamenyauka, hata mizabibu ya Sibuma iliyoleta zabibu zenye mvinyo kali za kulevya nao wakuu wa wamizimu; matawi yao yaliendelea sana, yakafika Yazeri, mengine yakapotea nyikani, miche yao ikaenea po pote mpaka kwenye bahari.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Maana makonde ya Heshboni yamenyauka, na mzabibu wa Sibma; mabwana wa mataifa wameyavunja matawi yake mateule; yamefika hata Yazeri, yalitanga-tanga hata nyikani; matawi yake yalitapakaa, yaliivuka bahari.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Mashamba ya Hesiboni yamefifia, vilevile na zabibu za Sibuma ambazo ziliwalewesha wakubwa wa mataifa. Zikafika Yaweri na kusambaa hata katika jangwa, chipukizi zake zikafika hata ngambo ya bahari.