Isaiah 16:9 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Kwa hiyo ninalia pamoja na Yazeri kwa ajili ya mizabibu ya Sibma. Machozi yananitoka kwa ajili yenu, enyi miji ya Heshboni na Eleale; maana vigelegele vya mavuno ya matunda, vigelegele vya mavuno ya nafaka vimetoweka.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Hivyo ninalia kama Yazeri aliavyo, kwa ajili ya mizabibu ya Sibma. Ee Heshboni, ee Eleale, ninakulowesha kwa machozi! Shangwe za furaha kwa ajili ya tunda lako lililoiva na kwa ajili ya mavuno zimekomeshwa.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Basi, naililia mizabibu ya Sibma kwa kilio cha Yazeri, nitawanyeshea machozi yangu, Ee Heshboni na Eleale, kwa kuwa kelele za vita zimeyaangukia mavuno ya matunda yako, na mavuno ya mizabibu yako.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Kwa hiyo ninalia pamoja na Yazeri kwa ajili ya mizabibu ya Sibma. Machozi yananitoka kwa ajili yenu, enyi miji ya Heshboni na Eleale; maana vigelegele vya mavuno ya matunda, vigelegele vya mavuno ya nafaka vimetoweka.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Hivyo ninalia kama Yazeri aliavyo, kwa ajili ya mizabibu ya Sibma. Ee Heshboni, Ee Eleale, ninakulowesha kwa machozi! Kelele za furaha kwa ajili ya tunda lako lililoiva na kwa ajili ya mavuno zimekomeshwa.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Hivyo ninalia kama Yazeri aliavyo, kwa ajili ya mizabibu ya Sibma. Ee Heshboni, ee Eleale, ninakulowesha kwa machozi! Kelele za furaha kwa ajili ya tunda lako lililoiva na kwa ajili ya mavuno zimekomeshwa.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Basi, naililia mizabibu ya Sibma kwa kilio cha Yazeri, nitawanyeshea machozi yangu, Ee Heshboni na Eleale, kwa kuwa kelele za vita zimeyaangukia mavuno ya matunda yako, na mavuno ya mizabibu yako.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Kwa hiyo ninalia pamoja na Yazeri kwa ajili ya mizabibu ya Sibma. Machozi yananitoka kwa ajili yenu, enyi miji ya Heshboni na Eleale; maana vigelegele vya mavuno ya matunda, vigelegele vya mavuno ya nafaka vimetoweka.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kwa hiyo nami ninaililia mizabibu ya Sibuma pamoja na watu wa Yazeri, machozi yangu yazinyeshee nchi za Hesiboni na za Elale, kwani mazomeo yamewaangukia siku hizi za kiangazi zilizo siku zenu za mavuno yenu.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Basi, naililia mizabibu ya Sibma kwa kilio cha Yazeri, nitawanyeshea machozi yangu, Ee Heshboni na Eleale, kwa kuwa kelele za vita zimeyaangukia mavuno ya matunda yako, na mavuno ya mizabibu yako.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Kwa hiyo ninalia pamoja na Yaweri kwa ajili ya mizabibu ya Sibuma. Machozi yananitoka kwa ajili yenu, enyi miji ya Hesiboni na Eleale; maana vigelegele vya mavuno ya matunda na ya ngano vimetoweka.