Isaiah 17:13 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Mataifa yananguruma kama ngurumo ya maji mengi, lakini Mungu atayakemea, nayo yatakimbilia mbali. Yatafukuzwa kama makapi mlimani mbele ya upepo; kama vumbi litimuliwalo na kimbunga.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Ingawa mataifa yanavuma kama ngurumo za maji yanayofanya mawimbi, wakati anayakemea yanakimbia mbali, yanafukuzwa mbele ya upepo kama makapi juu ya milima, kama jani likivingirishwa na dhoruba.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Mataifa wananguruma kama ngurumo ya maji mengi; Lakini atawakemea, nao watakimbia mbali sana, Watafukuzwa kama makapi milimani mbele ya upepo, Na kama mavumbi vuruvuru mbele ya tufani.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Mataifa yananguruma kama ngurumo ya maji mengi, lakini Mungu atayakemea, nayo yatakimbilia mbali. Yatafukuzwa kama makapi mlimani mbele ya upepo; kama vumbi litimuliwalo na kimbunga.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Ingawa mataifa yanavuma kama ngurumo za maji yanayofanya mawimbi, wakati anapoyakemea yanakimbia mbali, yanafukuzwa mbele ya upepo kama makapi juu ya milima, kama jani livingirishwapo na dhoruba.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Ingawa mataifa yanavuma kama ngurumo za maji yanayofanya mawimbi, wakati anapoyakemea yanakimbia mbali, yanafukuzwa mbele ya upepo kama makapi juu ya milima, kama jani livingirishwapo na dhoruba.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Mataifa wananguruma kama ngurumo ya maji mengi; Lakini atawakemea, nao watakimbia mbali sana, Watafukuzwa kama makapi milimani mbele ya upepo, Na kama mavumbi vuruvuru mbele ya tufani.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Mataifa yananguruma kama ngurumo ya maji mengi, lakini Mungu atayakemea, nayo yatakimbilia mbali. Yatafukuzwa kama makapi mlimani mbele ya upepo; kama vumbi litimuliwalo na kimbunga.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Lakini ijapo makabila ya watu yangurume, kama maji mengi yanavyonguruma, yeye atakapowakaripia, watakimbia mbali sana, watafukuzwa, waruke kama makapi, yakipeperushwa na upepo vilimani juu, au kama mavumbi, yakichukuliwa na kimbunga.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Mataifa wananguruma kama ngurumo ya maji mengi; Lakini atawakemea, nao watakimbia mbali sana, Watafukuzwa kama makapi milimani mbele ya upepo, Na kama mavumbi vuruvuru mbele ya tufani.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Mataifa yananguruma kama ngurumo ya maji mengi, lakini Mungu atayakaripia, nayo yatakimbilia mbali. Yatafukuzwa kama maganda juu ya mulima mbele ya upepo; kama mavumbi yanayonyanyuliwa na upepo mukali.