Isaiah 17:3 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Ngome za kujihami za Efraimu zitatoweka, na utawala wa Damasko utakwisha. Waashuru ambao watabaki hai, watakuwa na fedheha kama wazawa wa Israeli. Mimi Mwenyezi-Mungu wa majeshi nimenena.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Mji wenye ngome utatoweka kutoka Efraimu, nao uweza wa ufalme kutoka Dameski; mabaki ya Aramu yatakuwa kama utukufu wa Waisraeli,” asema Mwenyezi Mungu, Mungu wa majeshi ya mbinguni.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Na ngome ya Efraimu itakomeshwa, na ufalme wa Dameski, na mabaki ya Shamu; watakuwa kama utukufu wa wana wa Israeli, asema Bwana wa majeshi.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Ngome za kujihami za Efraimu zitatoweka, na utawala wa Damasko utakwisha. Waashuru ambao watabaki hai, watakuwa na fedheha kama wazawa wa Israeli. Mimi Mwenyezi-Mungu wa majeshi nimenena.”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Mji wenye ngome utatoweka kutoka Efraimu, nao uweza wa kifalme kutoka Dameski; mabaki ya Aramu yatakuwa kama utukufu wa Waisraeli,” asema BWANA Mwenye Nguvu Zote.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Mji wenye ngome utatoweka kutoka Efraimu, nao uweza wa ufalme kutoka Dameski; mabaki ya Aramu yatakuwa kama utukufu wa Waisraeli,” asema bwana Mwenye Nguvu Zote.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Na ngome ya Efraimu itakomeshwa, na ufalme wa Dameski, na mabaki ya Shamu; watakuwa kama utukufu wa wana wa Israeli, asema BWANA wa majeshi.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Ngome za kujihami za Efraimu zitatoweka, na utawala wa Damasko utakwisha. Waashuru ambao watabaki hai, watakuwa na fedheha kama wazawa wa Israeli. Mimi Mwenyezi-Mungu wa majeshi nimenena.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Hivyo ngome ya Efuraimu itapotea, ufalme utakapoondoka Damasko, nalo sao la Ushami litakuwa kama utukufu wa Waisiraeli; ndivyo, asemavyo Bwana Mwenye vikosi.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Na ngome ya Efraimu itakomeshwa, na ufalme wa Dameski, na mabaki ya Shamu; watakuwa kama utukufu wa wana wa Israeli, asema BWANA wa majeshi.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Pango za Efuraimu zitatoweka, na utawala wa Damasiki utakwisha. Waaramu ambao watabaki wazima, hawatakuwa na utukufu zaidi kama wazao wa Israeli. –Ni ujumbe wa Yawe wa majeshi.