Isaiah 17:5 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Atakwisha kama shamba lililovunwa, atafanyiwa kama mvunaji avunavyo nafaka, atakuwa kama shamba lililovunwa bondeni Refaimu.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Itakuwa kama mvunaji akusanyavyo nafaka na kuvuna nafaka kwa mikono yake, kama wakati mtu aokotapo masazo ya masuke katika Bonde la Warefai.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Tena itakuwa kama hapo avunaye ashikapo mabua ya ngano, na mkono wake ukatapo masuke; tena itakuwa kama hapo mtu aokotapo masuke katika bonde la Warefai.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Atakwisha kama shamba lililovunwa, atafanyiwa kama mvunaji avunavyo nafaka, atakuwa kama shamba lililovunwa bondeni Refaimu.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Itakuwa kama mvunaji akusanyavyo nafaka na kuvuna nafaka kwa mikono yake, kama wakati mtu aokotapo masazo ya masuke ya nafaka katika Bonde la Warefai.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Itakuwa kama mvunaji akusanyavyo nafaka na kuvuna nafaka kwa mikono yake, kama wakati mtu aokotapo masazo ya masuke katika Bonde la Warefai.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Tena itakuwa kama hapo mvunaji ashikapo mabua ya ngano, na mkono wake ukatapo masuke; tena itakuwa kama hapo mtu aokotapo masuke katika bonde la Warefai.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Atakwisha kama shamba lililovunwa, atafanyiwa kama mvunaji avunavyo nafaka, atakuwa kama shamba lililovunwa bondeni Refaimu.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Itakuwa kama mvunaji akishika manyasi, mkono wake ukate masuke, au itakuwa kama mtu akitaka kuokota masuke katika bonde la Refaimu.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Tena itakuwa kama hapo avunaye ashikapo mabua ya ngano, na mkono wake ukatapo masuke; tena itakuwa kama hapo mtu aokotapo masuke katika bonde la Warefai.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Itakuwa kama wakati wa mavuno, wakati wamekwisha kuokota ngano, na kukusanya masuke katika mukono. Hakika, itakuwa kama bonde la Refaimu wakati wamekwisha kuvuna ngano.