Isaiah 17:6 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Atabakiziwa wachache kama vile baada ya zeituni: Zeituni mbili, tatu katika tawi la juu; nne, tano katika matawi ya mti uzaao sana. Mimi Mwenyezi-Mungu, Mungu wa Israeli, nimenena.”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Hata hivyo baadhi ya masazo yatabaki, kama vile mti wa mzeituni unavyopigwa, kukiachwa zeituni mbili au tatu juu ya matawi kileleni, nne au tano katika matawi yanayozaa sana,” asema Mwenyezi Mungu, Mungu wa Israeli.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Lakini kilichosazwa na mvunaji kitakuwa ndani yake, kama vile wakati wa kupiga mizeituni, matunda mawili matatu yaliyo juu sana; matunda manne matano katika matawi, matawi ya mti wa matunda, asema Bwana, Mungu wa Israeli.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Atabakiziwa wachache kama vile baada ya zeituni: Zeituni mbili, tatu katika tawi la juu; nne, tano katika matawi ya mti uzaao sana. Mimi Mwenyezi-Mungu, Mungu wa Israeli, nimenena.”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Hata hivyo baadhi ya masazo yatabaki, kama vile mti wa mzeituni unavyopigwa, kukiachwa zeituni mbili au tatu juu ya matawi ya kileleni, nne au tano katika matawi yazaayo sana,” asema BWANA, Mungu wa Israeli.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Hata hivyo baadhi ya masazo yatabaki, kama vile mti wa mzeituni unavyopigwa, kukiachwa zeituni mbili au tatu juu ya matawi kileleni, nne au tano katika matawi yazaayo sana,” asema bwana, Mungu wa Israeli.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Lakini kilichosazwa na mvunaji kitakuwa ndani yake, kama vile wakati wa kupiga mizeituni, matunda mawili matatu yaliyo juu sana; matunda manne matano katika matawi, matawi ya mti wa matunda, asema BWANA, Mungu wa Israeli.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Atabakiziwa wachache kama vile baada ya zeituni: Zeituni mbili, tatu katika tawi la juu; nne, tano katika matawi ya mti uzaao sana. Mimi Mwenyezi-Mungu, Mungu wa Israeli, nimenena.”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Watakaosalia watakuwa wa kuokoteza, itakuwa kama penye mavuno ya matunda ya mchekele: mawili matatu yatasalia kileleni juu kabisa, manne matano yatasalia katika matawi ya mti, ulioyazaa; ndivyo, asemavyo Bwana Mungu wa Isiraeli.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Lakini kilichosazwa na mvunaji kitakuwa ndani yake, kama vile wakati wa kupiga mizeituni, matunda mawili matatu yaliyo juu sana; matunda manne matano katika matawi, matawi ya mti wa matunda, asema BWANA, Mungu wa Israeli.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Watabaki wachache kama vile kisha kuangusha matunda ya mizeituni: matunda mawili au matatu katika tawi la juu; mane, matano katika matawi yanayozaa sana. –Ni ujumbe wa Yawe, Mungu wa Israeli.