Isaiah 18:2 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Inatuma wajumbe ambao wanasafiri mtoni Nili, wamepanda mashua za mafunjo. Nendeni, enyi wajumbe wepesi, kwa taifa kubwa na hodari, la watu warefu na wa ngozi laini. Watu hao wanaoogopwa kila mahali na nchi yao imegawanywa na mito.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
iwapelekayo wajumbe wake kupitia bahari kwa mashua za mafunjo juu ya maji. Nendeni, wajumbe wepesi, kwa taifa la watu warefu wenye ngozi nyororo, kwa taifa linaloogopwa mbali na karibu, taifa gomvi lenye lugha ngeni, ambalo nchi yao imegawanywa kwa mito.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Ipelekayo wajumbe wake kwa njia ya bahari, Na katika vyombo vya manyasi juu ya maji.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Inatuma wajumbe ambao wanasafiri mtoni Nili, wamepanda mashua za mafunjo. Nendeni, enyi wajumbe wepesi, kwa taifa kubwa na hodari, la watu warefu na wa ngozi laini. Watu hao wanaoogopwa kila mahali na nchi yao imegawanywa na mito.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
iwapelekayo wajumbe wake kwa njia ya bahari kwa mashua za mafunjo juu ya maji. Nendeni, wajumbe wepesi, kwa taifa la watu warefu wenye ngozi nyororo, kwa taifa linaloogopwa mbali na karibu, taifa gomvi lenye lugha ngeni, ambalo nchi yao imegawanywa kwa mito.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
iwapelekayo wajumbe wake kwa njia ya bahari kwa mashua za mafunjo juu ya maji. Nendeni, wajumbe wepesi, kwa taifa la watu warefu wenye ngozi nyororo, kwa taifa linaloogopwa mbali na karibu, taifa gomvi lenye lugha ngeni, ambalo nchi yao imegawanywa kwa mito.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Ipelekayo wajumbe wake kwa njia ya bahari, Na katika vyombo vya manyasi juu ya maji. Nendeni, wajumbe wepesi, kwa watu warefu, laini; Watu watishao tangu mwanzo wao hata sasa; Taifa la wenye nguvu, wakanyagao watu, Ambao mito inakata nchi yao.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Inatuma wajumbe ambao wanasafiri mtoni Nili, wamepanda mashua za mafunjo. Nendeni, enyi wajumbe wepesi, kwa taifa kubwa na hodari, la watu warefu na wa ngozi laini. Watu hao wanaoogopwa kila mahali na nchi yao imegawanywa na mito.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Ninyi wajumbe mliokuja mkilifuata lile jito kubwa katika mitumbwi yenu ya mafunjo ya kwendea juu ya maji, ninyi wajumbe wepesi, nendeni kwenu kwenye watu warefu sana wajipakao mafuta. Ndio watu wanaoogopwa kwao hata kungineko, kwa kuwa ni wenye nguvu za kuponda watu, nayo nchi yao inakatwakatwa na mito.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Ipelekayo wajumbe wake kwa njia ya bahari, Na katika vyombo vya manyasi juu ya maji. Nendeni, wajumbe wepesi, kwa watu warefu, laini; Watu watishao tangu mwanzo wao hata sasa; Taifa la wenye nguvu, wakanyagao watu, Ambao mito inakata nchi yao.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Inatuma wajumbe ambao wanasafiri ndani ya muto Nili, wamepanda ndani ya mitumbwi iliyotengenezwa na matete. Muende, enyi wajumbe wepesi, kwa taifa kubwa na hodari, la watu warefu wenye ngozi laini, wanaotisha kwa karibu na kwa mbali, taifa la watu wenye nguvu na ushindi, ambalo inchi yake imegawanywa na mito.