Isaiah 18:7 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Wakati huo, Mwenyezi-Mungu wa majeshi ataletewa tambiko kutoka kwa watu warefu wenye ngozi laini, watu watishao karibu na mbali, taifa la watu wenye nguvu na ushindi, ambalo ardhi yake imegawanywa na mito. Ataletewa tambiko hizo mlimani Siyoni anapoabudiwa yeye Mwenyezi-Mungu wa majeshi.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Wakati huo matoleo yataletwa kwa Mwenyezi Mungu, Mungu wa majeshi ya mbinguni kutoka kwa taifa la watu warefu wenye ngozi nyororo, kutoka kwa taifa linaloogopwa mbali na karibu, kutoka taifa gomvi lenye lugha ngeni, ambalo nchi yao imegawanywa kwa mito, matoleo yataletwa katika Mlima Sayuni, mahali pa Jina la Mwenyezi Mungu, Mungu wa majeshi ya mbinguni.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Wakati huo Bwana wa majeshi ataletewa hedaya na watu warefu, laini; Watu watishao tangu mwanzo wao hata sasa; Taifa la wenye nguvu, wakanyagao watu, Ambao mito inakata nchi yao;
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Wakati huo, Mwenyezi-Mungu wa majeshi ataletewa tambiko kutoka kwa watu warefu wenye ngozi laini, watu watishao karibu na mbali, taifa la watu wenye nguvu na ushindi, ambalo ardhi yake imegawanywa na mito. Ataletewa tambiko hizo mlimani Siyoni anapoabudiwa yeye Mwenyezi-Mungu wa majeshi.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Wakati huo matoleo yataletwa kwa BWANA Mwenye Nguvu Zote kutoka kwa taifa la watu warefu wenye ngozi nyororo, kutoka kwa taifa linaloogopwa mbali na karibu, kutoka taifa gomvi lenye lugha ngeni, ambalo nchi yao imegawanywa kwa mito, matoleo yataletwa katika Mlima Sayuni, mahali pa Jina la BWANA Mwenye Nguvu Zote.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Wakati huo matoleo yataletwa kwa bwana Mwenye Nguvu Zote kutoka kwa taifa la watu warefu wenye ngozi nyororo, kutoka kwa taifa linaloogopwa mbali na karibu, kutoka taifa gomvi lenye lugha ngeni, ambalo nchi yao imegawanywa kwa mito, matoleo yataletwa katika Mlima Sayuni, mahali pa Jina la bwana Mwenye Nguvu Zote.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Wakati huo BWANA wa majeshi ataletewa hidaya na watu warefu, laini; Watu watishao tangu mwanzo wao hata sasa; Taifa la wenye nguvu, wakanyagao watu, Ambao mito inagawanya nchi yao; Mpaka mahali pa jina la BWANA wa majeshi, mlima Sayuni.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Wakati huo, Mwenyezi-Mungu wa majeshi ataletewa tambiko kutoka kwa watu warefu wenye ngozi laini, watu watishao karibu na mbali, taifa la watu wenye nguvu na ushindi, ambalo ardhi yake imegawanywa na mito. Ataletewa tambiko hizo mlimani Siyoni anapoabudiwa yeye Mwenyezi-Mungu wa majeshi.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Siku zile Bwana Mwenye vikosi ataletewa matunzo nao walio watu warefu sana wajipakao mafuta. Ndio wale watu wanaoogopwa kwao na kungineko, kwa kuwa ni watu wenye nguvu za kuponda watu, nayo nchi yao inakatwakatwa na mito. Hao watatua matunzo yao mahali penye Jina la Bwana Mwenye vikosi, ndipo mlimani kwa Sioni.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Wakati huo BWANA wa majeshi ataletewa hedaya na watu warefu, laini; Watu watishao tangu mwanzo wao hata sasa; Taifa la wenye nguvu, wakanyagao watu, Ambao mito inakata nchi yao; Mpaka mahali pa jina la BWANA wa majeshi, mlima Sayuni.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Wakati huo, Yawe wa majeshi ataletewa sadaka kutoka kwa watu warefu na wenye ngozi laini, watu wanaotisha kwa karibu na kwa mbali, taifa la watu wenye nguvu na ushindi, ambalo inchi yake imegawanywa na mito. Ataletewa sadaka hizo kwenye mulima Sayuni anapoabudiwa yeye Yawe wa majeshi.