Isaiah 19:1 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Kauli ya Mungu dhidi ya nchi ya Misri. “Mwenyezi-Mungu amepanda juu ya wingu liendalo kasi na kuja mpaka nchi ya Misri. Sanamu za miungu ya Wamisri zitatetemeka mbele yake, mioyo ya Wamisri itayeyuka kwa hofu.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Neno la unabii kuhusu Misri: Tazama, Mwenyezi Mungu amepanda juu ya wingu liendalo kwa haraka naye anakuja Misri. Sanamu za Misri zinatetemeka mbele yake, nayo mioyo ya Wamisri inayeyuka ndani yao.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Ufunuo juu ya Misri. Tazama, Bwana amepanda juu ya wingu jepesi, anafika Misri; na sanamu za Misri zinatikisika mbele zake, na moyo wa Misri unayeyuka ndani yake.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Kauli ya Mungu dhidi ya nchi ya Misri. “Mwenyezi-Mungu amepanda juu ya wingu liendalo kasi na kuja mpaka nchi ya Misri. Sanamu za miungu ya Wamisri zitatetemeka mbele yake, mioyo ya Wamisri itayeyuka kwa hofu.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Neno kuhusu Misri: Tazama, BWANA amepanda juu ya wingu liendalo kwa haraka naye anakuja Misri. Sanamu za Misri zinatetemeka mbele yake, nayo mioyo ya Wamisri inayeyuka ndani yao.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Neno kuhusu Misri: Tazama, bwana amepanda juu ya wingu liendalo kwa haraka naye anakuja Misri. Sanamu za Misri zinatetemeka mbele yake, nayo mioyo ya Wamisri inayeyuka ndani yao.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Ufunuo juu ya Misri. Tazama, BWANA amepanda juu ya wingu jepesi, anafika Misri; na sanamu za Misri zinatikisika mbele zake, na moyo wa Misri unayeyuka ndani yake.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Kauli ya Mungu dhidi ya nchi ya Misri. “Mwenyezi-Mungu amepanda juu ya wingu liendalo kasi na kuja mpaka nchi ya Misri. Sanamu za miungu ya Wamisri zitatetemeka mbele yake, mioyo ya Wamisri itayeyuka kwa hofu.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Tazameni: Bwana amepanda wingu jepesi, aje Misri! Vinyago vya Misri vinatikisika usoni pake, mioyo yao Wamisri imeyeyuka vifuani mwao.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Ufunuo juu ya Misri. Tazama, BWANA amepanda juu ya wingu jepesi, anafika Misri; na sanamu za Misri zinatikisika mbele zake, na moyo wa Misri unayeyuka ndani yake.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Ujumbe wa Mungu juu ya inchi ya Misri. Yawe amepanda juu ya wingu linaloenda mbio na kuja mpaka katika inchi ya Misri. Sanamu za miungu ya Wamisri zitatetemeka mbele yake, mioyo ya Wamisri itayeyuka kwa woga.