Isaiah 19:11 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Viongozi wa mji wa Soani ni wapumbavu kabisa, washauri wa Farao wanatoa shauri la kijinga! Awezaje kila mmoja kumwambia Farao, “Mimi ni mzawa wa mtaalamu stadi; mzawa wa wafalme wa hapo kale!”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Maafisa wa Soani ni wapumbavu kabisa, washauri wa Farao wenye busara wanatoa ushauri wa kijinga. Unawezaje kumwambia Farao, “Mimi ni mmoja wa watu wenye hekima, mwanafunzi wa wafalme wa zamani”?
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Wakuu wa Soani wamekuwa wapumbavu kabisa; washauri wenye hekima wa Farao, shauri lao limepumbazika; mwawezaje kumwambia Farao, Mimi ni mwana wa wenye hekima, ni mwana wa wafalme wa zamani?
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Viongozi wa mji wa Soani ni wapumbavu kabisa, washauri wa Farao wanatoa shauri la kijinga! Awezaje kila mmoja kumwambia Farao, “Mimi ni mzawa wa mtaalamu stadi; mzawa wa wafalme wa hapo kale!”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Maafisa wa Soani ni wapumbavu kabisa, washauri wa Farao wenye busara wanatoa ushauri wa kijinga. Unawezaje kumwambia Farao, “Mimi ni mmojawapo wa watu wenye hekima, mwanafunzi wa wafalme wa zamani”?
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Maafisa wa Soani ni wapumbavu kabisa, washauri wa Farao wenye busara wanatoa ushauri wa kijinga. Unawezaje kumwambia Farao, “Mimi ni mmojawapo wa watu wenye hekima, mwanafunzi wa wafalme wa zamani”?
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Wakuu wa Soani wamekuwa wapumbavu kabisa; washauri wenye hekima wa Farao, ushauri wao umepumbazika; mwawezaje kumwambia Farao, Mimi ni mwana wa wenye hekima, ni mwana wa wafalme wa zamani?
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Viongozi wa mji wa Soani ni wapumbavu kabisa, washauri wa Farao wanatoa shauri la kijinga! Awezaje kila mmoja kumwambia Farao, “Mimi ni mzawa wa mtaalamu stadi; mzawa wa wafalme wa hapo kale!”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Wakuu wa Soani watakuwa wamepumbaa kabisa; nao wajuzi wa Farao wasiokosa mizungu, hapo mizungu yao itakuwa ujinga tu. Mtawezaje kumwambia Farao: Mimi ni mwana wao watambuzi? au: Mimi ni mwana wao wafalme wa kale?
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Wakuu wa Soani wamekuwa wapumbavu kabisa; washauri wenye hekima wa Farao, shauri lao limepumbazika; mwawezaje kumwambia Farao, Mimi ni mwana wa wenye hekima, ni mwana wa wafalme wa zamani?
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Wakubwa wa muji wa Soani ni wapumbafu kabisa, washauri wa Mufalme wa Misri wanatoa shauri la kijinga! Kila mumoja anaweza namna gani kumwambia Mufalme wa Misri: Mimi ni wa uzao wa wenye hekima, wa uzao wa wafalme wa zamani!