Isaiah 19:17 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Yuda atakuwa tishio kubwa kwa Wamisri. Wote watakaoambiwa habari za Yuda wataingiwa na woga kwa sababu ya jambo aliloamua Mwenyezi-Mungu wa majeshi kuwatenda.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Nayo nchi ya Yuda itawatia hofu Wamisri, kila mmoja atakayetajiwa Yuda ataingiwa na hofu, kwa sababu ya kile ambacho Mwenyezi Mungu, Mungu wa majeshi ya mbinguni anapanga dhidi yao.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Na nchi ya Yuda itakuwa sababu ya utisho kwa Misri; kila mtu atakayeambiwa habari zake ataingiwa na woga, kwa sababu ya kusudi la Bwana wa majeshi, analolikusudia juu yake.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Yuda atakuwa tishio kubwa kwa Wamisri. Wote watakaoambiwa habari za Yuda wataingiwa na woga kwa sababu ya jambo aliloamua Mwenyezi-Mungu wa majeshi kuwatenda.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Nayo nchi ya Yuda itawatia hofu Wamisri, kila mmoja atakayetajiwa Yuda ataingiwa na hofu, kwa sababu ya kile ambacho BWANA Mwenye Nguvu Zote anapanga dhidi yao.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Nayo nchi ya Yuda itawatia hofu Wamisri, kila mmoja atakayetajiwa Yuda ataingiwa na hofu, kwa sababu ya kile ambacho bwana Mwenye Nguvu Zote anapanga dhidi yao.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Na nchi ya Yuda itakuwa kitisho kwa Misri; kila mtu atakayeambiwa habari zake ataingiwa na woga, kwa sababu ya kusudi la BWANA wa majeshi, analolikusudia juu yake.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Yuda atakuwa tishio kubwa kwa Wamisri. Wote watakaoambiwa habari za Yuda wataingiwa na woga kwa sababu ya jambo aliloamua Mwenyezi-Mungu wa majeshi kuwatenda.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Hapo nchi ya Yuda itawawia Wamisri kitisho, kila mtu aingiwe na kituko atakaposikia, ikitajwa, kwa ajili ya shauri la Bwana Mwenye vikosi, alilowakatia.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Na nchi ya Yuda itakuwa sababu ya utisho kwa Misri; kila mtu atakayeambiwa habari zake ataingiwa na woga, kwa sababu ya kusudi la BWANA wa majeshi, analolikusudia juu yake.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Yuda atakuwa kitisho kikubwa kwa Wamisri. Wote watakaoambiwa habari za Yuda wataingiwa na woga kwa sababu ya jambo Yawe wa majeshi aliloamua kuwatendea.