Isaiah 19:18 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Siku hiyo lugha ya Kiebrania itatumika katika miji mitano ya Misri, na watu wa miji hiyo wataapa kuwa waaminifu kwa Mwenyezi-Mungu wa majeshi. Mji mmojawapo utaitwa “Mji wa Jua.”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Katika siku hiyo miji mitano ya Misri, itazungumza lugha ya Kanaani, na kuapa kumtii Mwenyezi Mungu, Mungu wa majeshi ya mbinguni. Mji mmoja utaitwa Mji wa Uharibifu.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Katika siku hiyo itakuwako miji mitano katika nchi ya Misri itumiayo lugha ya Kanaani, na kumwapia Bwana wa majeshi; mji mmoja utaitwa Mji wa uharibifu.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Siku hiyo lugha ya Kiebrania itatumika katika miji mitano ya Misri, na watu wa miji hiyo wataapa kuwa waaminifu kwa Mwenyezi-Mungu wa majeshi. Mji mmojawapo utaitwa “Mji wa Jua.”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Katika siku hiyo miji mitano ya Misri itazungumza lugha ya Kanaani na kuapa kumtii BWANA Mwenye Nguvu Zote. Mji mmojawapo utaitwa Mji wa Uharibifu.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Katika siku hiyo miji mitano ya Misri, itazungumza lugha ya Kanaani, na kuapa kumtii bwana Mwenye Nguvu Zote. Mji mmojawapo utaitwa Mji wa Uharibifu.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Katika siku hiyo itakuwako miji mitano katika nchi ya Misri itumiayo lugha ya Kanaani, na kumwapia BWANA wa majeshi; mji mmoja utaitwa Mji wa jua.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Siku hiyo lugha ya Kiebrania itatumika katika miji mitano ya Misri, na watu wa miji hiyo wataapa kuwa waaminifu kwa Mwenyezi-Mungu wa majeshi. Mji mmojawapo utaitwa “Mji wa Jua.”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Siku ile miji mitano itakuwako katika nchi ya Misri itakayosema msemo wa Kanaani, itakayoapa na kulitaja Jina la Bwana Mwenye vikosi, mmoja wao utaitwa Mji wa Mabomoko.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Katika siku hiyo itakuwako miji mitano katika nchi ya Misri itumiayo lugha ya Kanaani, na kumwapia BWANA wa majeshi; mji mmoja utaitwa Mji wa uharibifu.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Siku hiyo luga ya Kiebrania itatumika katika miji mitano ya Misri, na watu wa miji hiyo wataapa kuwa waaminifu kwa Yawe wa majeshi. Muji mumoja kati ya miji hiyo utaitwa “Muji wa Jua”.