Isaiah 19:20 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Madhabahu hiyo itakuwa ishara na ushuhuda kwake Mwenyezi-Mungu wa majeshi katika nchi ya Misri. Watu wakimlilia Mwenyezi-Mungu humo kwa sababu ya kukandamizwa, yeye atawapelekea mkombozi atakayewatetea na kuwakomboa.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Itakuwa alama na ushahidi kwa ajili ya Mwenyezi Mungu, Mungu wa majeshi ya mbinguni katika nchi ya Misri. Watakapomlilia Mwenyezi Mungu kwa sababu ya watesi wao, Mungu atawapelekea mwokozi na mtetezi, naye atawaokoa.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Nayo itakuwa ishara na ushuhuda kwa Bwana wa majeshi katika nchi ya Misri; kwa maana watamlilia Bwana kwa sababu ya watu wawaoneao, naye atawapelekea mwokozi mwenye kuwatetea, naye atawaokoa.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Madhabahu hiyo itakuwa ishara na ushuhuda kwake Mwenyezi-Mungu wa majeshi katika nchi ya Misri. Watu wakimlilia Mwenyezi-Mungu humo kwa sababu ya kukandamizwa, yeye atawapelekea mkombozi atakayewatetea na kuwakomboa.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Itakuwa alama na ushahidi kwa ajili ya BWANA Mwenye Nguvu Zote katika nchi ya Misri. Watakapomlilia BWANA kwa sababu ya watesi wao, Mungu atawapelekea Mwokozi na mtetezi, naye atawaokoa.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Itakuwa alama na ushahidi kwa ajili ya bwana Mwenye Nguvu Zote katika nchi ya Misri. Watakapomlilia bwana kwa sababu ya watesi wao, Mungu atawapelekea mwokozi na mtetezi, naye atawaokoa.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Nayo itakuwa ishara na ushuhuda kwa BWANA wa majeshi katika nchi ya Misri; kwa maana watamlilia BWANA kwa sababu ya watu wawaoneao, naye atawapelekea mwokozi wa kuwatetea, naye atawaokoa.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Madhabahu hiyo itakuwa ishara na ushuhuda kwake Mwenyezi-Mungu wa majeshi katika nchi ya Misri. Watu wakimlilia Mwenyezi-Mungu humo kwa sababu ya kukandamizwa, yeye atawapelekea mkombozi atakayewatetea na kuwakomboa.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Hivyo Bwana Mwenye vikosi atakuwa na kielekezo cha kumshuhudia katika nchi ya Misri; napo, watakapomlilia Bwana kwa ajili yao wawasongao, atatuma mwokozi, awagombee, awaponye.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Nayo itakuwa ishara na ushuhuda kwa BWANA wa majeshi katika nchi ya Misri; kwa maana watamlilia BWANA kwa sababu ya watu wawaoneao, naye atawapelekea mwokozi mwenye kuwatetea, naye atawaokoa.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Mazabahu hayo yatakuwa kitambulisho na ushuhuda kwa Yawe wa majeshi katika inchi ya Misri. Watu wakimulilia Yawe humo kwa sababu ya kugandamizwa, yeye atawapelekea mukombozi atakayewatetea na kuwakomboa.