Isaiah 19:21 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Mwenyezi-Mungu atajijulisha kwa Wamisri na hapo ndipo Wamisri watakapomkiri na kumwabudu kwa kumtolea tambiko na sadaka za kuteketezwa. Hali kadhalika, watamwekea Mwenyezi-Mungu nadhiri ambazo watazitimiza.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Hivyo Mwenyezi Mungu atajijulisha mwenyewe kwa Wamisri, nao katika siku hiyo watamkubali Mwenyezi Mungu. Wataabudu kwa kumtolea dhabihu na sadaka za nafaka, watamwekea Mwenyezi Mungu nadhiri na kuzitimiza.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Na Bwana atajulikana na Misri, na Wamisri watamjua Bwana katika siku hiyo; naam watamtumikia kwa dhabihu na matoleo, nao watamwekea Bwana nadhiri, na kuzitekeleza.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Mwenyezi-Mungu atajijulisha kwa Wamisri na hapo ndipo Wamisri watakapomkiri na kumwabudu kwa kumtolea tambiko na sadaka za kuteketezwa. Hali kadhalika, watamwekea Mwenyezi-Mungu nadhiri ambazo watazitimiza.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Hivyo BWANA atajijulisha mwenyewe kwa Wamisri, nao katika siku hiyo watamkubali BWANA. Wataabudu kwa kumtolea dhabihu na sadaka za nafaka, watamwekea BWANA nadhiri na kuzitimiza.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Hivyo bwana atajijulisha mwenyewe kwa Wamisri, nao katika siku hiyo watamkubali bwana. Wataabudu kwa kumtolea dhabihu na sadaka za nafaka, watamwekea bwana nadhiri na kuzitimiza.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Na BWANA atajulikana na Misri, na Wamisri watamjua BWANA katika siku hiyo; naam watamtumikia kwa dhabihu na matoleo, nao watamwekea BWANA nadhiri, na kuzitekeleza.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Mwenyezi-Mungu atajijulisha kwa Wamisri na hapo ndipo Wamisri watakapomkiri na kumwabudu kwa kumtolea tambiko na sadaka za kuteketezwa. Hali kadhalika, watamwekea Mwenyezi-Mungu nadhiri ambazo watazitimiza.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Ndivyo, Bwana atakavyojulikana kwa Wamisri, kweli Wamisri watamjua Bwana siku zile, watamtumikia na kumtolea ng'ombe za tambiko na vipaji vingine vya tambiko, nayo waliyomwagia Bwana kumpa, watayalipa.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Na BWANA atajulikana na Misri, na Wamisri watamjua BWANA katika siku hiyo; naam watamtumikia kwa dhabihu na matoleo, nao watamwekea BWANA nadhiri, na kuzitekeleza.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Yawe atajijulisha kwa Wamisri na hapo ndipo Wamisri watakapomwitikia na kumwabudu kwa kumutolea matoleo na sadaka za kuteketezwa. Vilevile watafanyia Yawe viapo ambavyo watavitimiza.