Isaiah 19:23 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Wakati huo, kutakuwa na barabara kuu kutoka nchi ya Misri hadi nchi ya Ashuru. Waashuru watawatembelea Wamisri, na Wamisri watawatembelea Waashuru; nao wote watamwabudu Mungu pamoja.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Katika siku hiyo kutakuwa na njia kuu kutoka Misri hadi Ashuru. Waashuru wataenda Misri, na Wamisri wataenda Ashuru. Wamisri na Waashuru wataabudu pamoja.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Katika siku hiyo itakuwako njia kuu itokayo Misri na kufika hata Ashuru; Mwashuri atafika Misri, na Mmisri atafika Ashuru, na Wamisri wataabudu pamoja na Waashuri.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Wakati huo, kutakuwa na barabara kuu kutoka nchi ya Misri hadi nchi ya Ashuru. Waashuru watawatembelea Wamisri, na Wamisri watawatembelea Waashuru; nao wote watamwabudu Mungu pamoja.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Katika siku hiyo kutakuwepo na njia kuu kutoka Misri hadi Ashuru. Waashuru watakwenda Misri na Wamisri watakwenda Ashuru. Wamisri na Waashuru wataabudu pamoja.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Katika siku hiyo kutakuwepo na njia kuu kutoka Misri hadi Ashuru. Waashuru watakwenda Misri, na Wamisri watakwenda Ashuru. Wamisri na Waashuru wataabudu pamoja.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Katika siku hiyo itakuwako njia kuu itokayo Misri na kufika hadi Ashuru; Mwashuri atafika Misri, na Mmisri atafika Ashuru, na Wamisri wataabudu pamoja na Waashuri.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Wakati huo, kutakuwa na barabara kuu kutoka nchi ya Misri hadi nchi ya Ashuru. Waashuru watawatembelea Wamisri, na Wamisri watawatembelea Waashuru; nao wote watamwabudu Mungu pamoja.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Siku zile itakuwako barabara toka Misri kwenda Asuri, nao Waasuri watakuja Misri, nao Wamisri watakuja Asuri kuamkiana, hivyo Wamisri na Waasuri watatumikiana.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Katika siku hiyo itakuwako njia kuu itokayo Misri na kufika hata Ashuru; Mwashuri atafika Misri, na Mmisri atafika Ashuru, na Wamisri wataabudu pamoja na Waashuri.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Wakati huo, kutakuwa barabara kubwa kutoka inchi ya Misri mpaka katika inchi ya Asuria. Waasuria watawatembelea Wamisri, na Wamisri watawatembelea Waasuria; nao wote watamwabudu Mungu pamoja.