Isaiah 19:3 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Nitawaondolea Wamisri uhodari wao, nitaivuruga mipango yao; watatafuta maoni kwa sanamu na mizimu, wachawi, mizuka na pepo.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Wamisri watakufa moyo, na nitaibatilisha mipango yao. Watatafuta ushauri kwa sanamu na kwa roho za waliokufa, kwa waaguzi na kwa wale waongeao na mizimu.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Na roho ya Misri itamwagika kabisa katikati yake, nami nitayabatilisha mashauri yake, nao watakwenda kwa sanamu zao, na kwa waganga, na kwa wapiga ramli, na kwa wachawi.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Nitawaondolea Wamisri uhodari wao, nitaivuruga mipango yao; watatafuta maoni kwa sanamu na mizimu, wachawi, mizuka na pepo.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Wamisri watakufa moyo, na nitaifanya mipango yao kuwa batili, watatafuta ushauri kwa sanamu na kwa roho za waliokufa, kwa wapiga ramli na kwa wale waongeao na mizimu.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Wamisri watakufa moyo, na nitaibatilisha mipango yao. Watatafuta ushauri kwa sanamu na kwa roho za waliokufa, kwa waaguzi na kwa wale waongeao na mizimu.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Na roho yao Misri itaondolewa, nami nitaiharibu mipango yao, nao watakwenda kwa sanamu zao, na kwa waganga, na kwa wapiga ramli na kwa wachawi.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Nitawaondolea Wamisri uhodari wao, nitaivuruga mipango yao; watatafuta maoni kwa sanamu na mizimu, wachawi, mizuka na pepo.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Hapo ndipo, roho zao Wamisri zitakapozimia vifuani mwao, nikiitengua mizungu yao; nao watatafuta msaada kwa vinyago na kwa waganga, kwa wachawi na kwa waaguaji.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Na roho ya Misri itamwagika kabisa katikati yake, nami nitayabatilisha mashauri yake, nao watakwenda kwa sanamu zao, na kwa waganga, na kwa wapiga ramli, na kwa wachawi.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Nitawaondolea Wamisri uhodari wao. Nitaivuruga mipango yao. Watatafuta shauri kwa sanamu na mizimu, wachawi, mizuka na pepo.