Isaiah 2:19 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Ingieni katika mapango miambani, katika mashimo ardhini, kuiepa hasira ya Mwenyezi-Mungu, mbali na utukufu wa enzi yake, atakapokuja kuitia hofu dunia.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Watu watakimbilia kwenye mapango ndani ya miamba, na kwenye mahandaki ardhini kutokana na utisho wa Mwenyezi Mungu na utukufu wa enzi yake, ainukapo kuitikisa dunia.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Na watu wataingia ndani ya pango za majabali, na ndani ya mashimo ya nchi, mbele za utisho wa Bwana na utukufu wa enzi yake, atakapoondoka ili aitetemeshe mno dunia.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Ingieni katika mapango miambani, katika mashimo ardhini, kuiepa hasira ya Mwenyezi-Mungu, mbali na utukufu wa enzi yake, atakapokuja kuitia hofu dunia.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Watu watakimbilia kwenye mapango ndani ya miamba na kwenye mahandaki ardhini kutokana na utisho wa BWANA na utukufu wa enzi yake, ainukapo kuitikisa dunia.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Watu watakimbilia kwenye mapango ndani ya miamba, na kwenye mahandaki ardhini kutokana na utisho wa bwana na utukufu wa enzi yake, ainukapo kuitikisa dunia.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Na watu wataingia ndani ya pango za majabali, na ndani ya mashimo ya nchi, mbele za utisho wa BWANA na utukufu wa enzi yake, atakapoondoka ili aitetemeshe mno dunia.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Ingieni katika mapango miambani, katika mashimo ardhini, kuiepa hasira ya Mwenyezi-Mungu, mbali na utukufu wa enzi yake, atakapokuja kuitia hofu dunia.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Ndipo, watakapokwenda mapangoni kwenye magenge namo mashimoni kwenye nchi kavu, wasiuone uso wa Bwana uwatishao wala utukufu wa ukuu wake, atakapoinuka kuistusha nchi.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Na watu wataingia ndani ya pango za majabali, na ndani ya mashimo ya nchi, mbele za utisho wa BWANA na utukufu wa enzi yake, atakapoondoka ili aitetemeshe mno dunia.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Muingie katika mapango chini ya mawe, katika mashimo ndani ya udongo, kwa kuepuka kitisho cha Yawe, mbali na mwangaza wa utukufu wake, atakapokuja kuogopesha dunia.