Isaiah 2:20 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Siku hiyo, watu watawatupia panya na popo vinyago vyao vya fedha na dhahabu walivyojitengenezea ili kuviabudu.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Siku ile, watu watawatupia panya na popo sanamu zao za fedha na za dhahabu, walizozitengeneza ili waziabudu.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Siku hiyo kila mtu atazitupilia mbali sanamu zake za fedha, na sanamu zake za dhahabu, walizojifanyia ili kuziabudu, kwa fuko na popo;
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Siku hiyo, watu watawatupia panya na popo vinyago vyao vya fedha na dhahabu walivyojitengenezea ili kuviabudu.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Katika siku ile watu watawatupia panya na popo vinyago vyao vya fedha na vya dhahabu, walivyovitengeneza ili waviabudu.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Siku ile, watu watawatupia panya na popo sanamu zao za fedha na za dhahabu, walizozitengeneza ili waziabudu.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Siku hiyo kila mtu atazitupilia mbali sanamu zake za fedha, na sanamu zake za dhahabu, walizojitengenezea ili kuziabudu, kwa fuko na popo;
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Siku hiyo, watu watawatupia panya na popo vinyago vyao vya fedha na dhahabu walivyojitengenezea ili kuviabudu.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Siku ile watu watavikupa vinyago vyao, ijapo viwe vya fedha na vya dhahabu; hivyo, walivyojifanyizia vya kuvitambikia, watavitupa kwenye panya na mapopo,
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Siku hiyo kila mtu atazitupilia mbali sanamu zake za fedha, na sanamu zake za dhahabu, walizojifanyia ili kuziabudu, kwa fuko na popo;
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Siku hiyo, watu watawatupia panya na popo sanamu za feza na zahabu walizojitengenezea kusudi waziabudu.