Isaiah 2:6 — Compare Translations

11 translations compared side by side

Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Sasa, ee Mungu, umewatupa watu wako, wazawa wa Yakobo. Maana kweli wachawi wa mashariki wamejaa kati yao, wapo na wapiga ramli kama kwa Wafilisti. Wanashirikiana na watu wageni.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Mwenyezi Mungu umewatelekeza watu wako, nyumba ya Yakobo. Wamejaa ushirikina unaotoka Mashariki, wanapiga ramli kama Wafilisti na wanashikana mikono na wapagani.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Maana wewe umewaacha watu wako, nyumba ya Israeli, kwa sababu wamejaa kawaida za mashariki, nao ni wapiga ramli kama Wafilisti, na wanapana mikono na wana wa wageni.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Sasa, ee Mungu, umewatupa watu wako, wazawa wa Yakobo. Maana kweli wachawi wa mashariki wamejaa kati yao, wapo na wapiga ramli kama kwa Wafilisti. Wanashirikiana na watu wageni.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Umewatelekeza watu wako, nyumba ya Yakobo. Wamejaa ushirikina utokao Mashariki, wanapiga ramli kama Wafilisti na wanashikana mikono na wapagani.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Umewatelekeza watu wako, nyumba ya Yakobo. Wamejaa ushirikina utokao Mashariki, wanapiga ramli kama Wafilisti na wanashikana mikono na wapagani.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Maana wewe umewaacha watu wako, nyumba ya Israeli, kwa sababu wamejaa kawaida za mashariki, nao ni wapiga ramli kama Wafilisti, na wanapeana mikono na wana wa wageni.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Sasa, ee Mungu, umewatupa watu wako, wazawa wa Yakobo. Maana kweli wachawi wa mashariki wamejaa kati yao, wapo na wapiga ramli kama kwa Wafilisti. Wanashirikiana na watu wageni.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kwani umewatupa wao waliokuwa ukoo wako, wale wa mlango wa Yakobo, kwani wamejaa mambo yatokayo maawioni kwa jua, huagulia mawingu kama Wafilisti, hufanya maagano nao vijana wa nchi ngeni.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Maana wewe umewaacha watu wako, nyumba ya Israeli, kwa sababu wamejaa kawaida za mashariki, nao ni wapiga ramli kama Wafilisti, na wanapana mikono na wana wa wageni.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Sasa, ee Mungu, umewatupa watu wako, wazao wa Yakobo. Maana kweli wachawi kutoka mashariki wamejaa kati yao; kuna waaguzi kama vile kwa Wafilistini. Wanashirikiana na watu wageni.