Isaiah 20:4 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Basi, mfalme wa Ashuru atawachukua mateka Wamisri na Wakushi, wakubwa kwa wadogo. Watachukuliwa, nao watatembea uchi na bila viatu; matako wazi, kwa aibu ya Misri.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
vivyo hivyo mfalme wa Ashuru atawaongoza mateka wa Wamisri, na watu wa uhamisho wa Kushi, uchi na bila viatu, vijana hata wazee, wakiwa matako wazi, kwa aibu ya Wamisri.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
vivyo hivyo mfalme wa Ashuru atawachukua uchi, wafungwa wa Misri, na watu wa Kushi waliohamishwa, watoto kwa wazee, hawana viatu, matako yao wazi, Misri iaibishwe.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Basi, mfalme wa Ashuru atawachukua mateka Wamisri na Wakushi, wakubwa kwa wadogo. Watachukuliwa, nao watatembea uchi na bila viatu; matako wazi, kwa aibu ya Misri.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
vivyo hivyo mfalme wa Ashuru atawaongoza mateka wa Wamisri na watu wa uhamisho wa Kushi uchi na bila viatu, vijana na wazee, wakiwa matako wazi, kwa aibu ya Wamisri.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
vivyo hivyo mfalme wa Ashuru atawaongoza mateka wa Wamisri, na watu wa uhamisho wa Kushi, uchi na bila viatu, vijana hata wazee, wakiwa matako wazi, kwa aibu ya Wamisri.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
vivyo hivyo mfalme wa Ashuru atawachukua uchi, wafungwa wa Misri, na watu wa Kushi waliohamishwa, watoto kwa wazee, bila viatu, matako yao wazi, Misri iaibishwe.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Basi, mfalme wa Ashuru atawachukua mateka Wamisri na Wakushi, wakubwa kwa wadogo. Watachukuliwa, nao watatembea uchi na bila viatu; matako wazi, kwa aibu ya Misri.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
ndivyo, mfalme wa Asuri atakavyopeleka mateka ya Misri nao Wanubi watakaokamatwa, vijana na wazee, waende wenye uchi vifuani na miguuni, hata matakoni, Wamisri watiwe soni.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
vivyo hivyo mfalme wa Ashuru atawachukua uchi, wafungwa wa Misri, na watu wa Kushi waliohamishwa, watoto kwa wazee, hawana viatu, matako yao wazi, Misri iaibishwe.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Basi, mufalme wa Asuria atawapeleka Wamisri na Wakushi kuwa wafungwa, wakubwa kama vile wadogo. Watapelekwa, nao watatembea uchi na bila viatu, matako wazi. Misri ipate haya!