Isaiah 21:1 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Kauli ya Mungu dhidi ya jangwa kando ya bahari. Kama vimbunga vinavyovuma kutoka kusini, wavamizi wanakuja kutoka jangwani, kutoka katika nchi ya kutisha.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Neno la unabii kuhusu Jangwa kando ya Bahari: Kama upepo wa kisulisuli unaopita katika nchi hadi kusini, mshambuliaji anakuja kutoka jangwani, kutoka nchi inayotisha.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Ufunuo juu ya bara ya bahari. Kama tufani za Negebu
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Kauli ya Mungu dhidi ya jangwa kando ya bahari. Kama vimbunga vinavyovuma kutoka kusini, wavamizi wanakuja kutoka jangwani, kutoka katika nchi ya kutisha.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Neno kuhusu Jangwa kando ya Bahari: Kama upepo wa kisulisuli unaopita katika nchi hadi kusini, mshambuliaji anakuja kutoka jangwani, kutoka katika nchi inayotisha.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Neno kuhusu Jangwa kando ya Bahari: Kama upepo wa kisulisuli unaopita katika nchi hadi kusini, mshambuliaji anakuja kutoka jangwani, kutoka nchi inayotisha.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Ufunuo juu ya nyika kando ya bahari. Kama tufani za Negebu zikaribiavyo kwa kasi, inakuja kutoka nyikani, toka nchi itishayo.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Kauli ya Mungu dhidi ya jangwa kando ya bahari. Kama vimbunga vinavyovuma kutoka kusini, wavamizi wanakuja kutoka jangwani, kutoka katika nchi ya kutisha.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kama upepo wenye nguvu unavyovuma upande wa kusini, ndivyo, mambo yanavyotoka nyikani katika nchi inayoogopwa.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Ufunuo juu ya bara ya bahari. Kama tufani za Negebu zikaribiavyo kwa kasi, inakuja kutoka bara, toka nchi itishayo.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Ujumbe wa Mungu juu ya jangwa kando ya bahari. Kama upepo mukali unaovuma kutoka kusini, washambulizi wanakuja kutokea katika jangwa, kutoka katika inchi ya kutisha.