Isaiah 21:3 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Kwa maono hayo nimeingiwa na hofu kubwa, uchungu mwingi umenikumba; kama uchungu wa mama anayejifungua. Maumivu yamenizidi hata siwezi kusikia; nimefadhaika hata siwezi kuona.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Kwa sababu hii, mwili wangu umeteswa na maumivu, maumivu makali ya ghafula yamenishika, kama yale ya mwanamke mwenye uchungu wa kuzaa. Nimeduwazwa na lile ninalolisikia, nimeshangazwa na lile ninaloliona.
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Kwa sababu hiyo viuno vyangu vimejaa maumivu, utungu umenishika, kama utungu wa mwanamke azaaye; ninaumwa sana, nisiweze kusikia; nimefadhaishwa wa hofu, nisiweze kuona.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Kwa maono hayo nimeingiwa na hofu kubwa, uchungu mwingi umenikumba; kama uchungu wa mama anayejifungua. Maumivu yamenizidi hata siwezi kusikia; nimefadhaika hata siwezi kuona.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Katika hili mwili wangu umeteswa na maumivu, maumivu makali ya ghafula yamenishika, kama yale ya mwanamke mwenye utungu wa kuzaa, nimeduwazwa na lile ninalolisikia, nimeshangazwa na lile ninaloliona.
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Katika hili mwili wangu umeteswa na maumivu, maumivu makali ya ghafula yamenishika, kama yale ya mwanamke mwenye utungu wa kuzaa. Nimeduwazwa na lile ninalolisikia, nimeshangazwa na lile ninaloliona.
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Kwa sababu hiyo viuno vyangu vimejaa maumivu, uchungu umenishika, kama uchungu wa mwanamke azaaye; ninaumwa sana, nisiweze kusikia; nimefadhaishwa kwa hofu, nisiweze kuona.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Kwa maono hayo nimeingiwa na hofu kubwa, uchungu mwingi umenikumba; kama uchungu wa mama anayejifungua. Maumivu yamenizidi hata siwezi kusikia; nimefadhaika hata siwezi kuona.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kwa hiyo viuno vyangu vimeenea kukauka, uchungu ukanishika kama uchungu wa mwanamke azaaye, kizunguzungu kikanipata, nisisikie, nikastushwa, nisione.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Kwa sababu hiyo viuno vyangu vimejaa maumivu, utungu umenishika, kama utungu wa mwanamke azaaye; ninaumwa sana, nisiweze kusikia; nimefadhaishwa wa hofu, nisiweze kuona.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Kwa maono hayo nimeingiwa na woga mukubwa. Maumivu mengi yamenishika, kama maumivu ya mama anayezaa. Nimefazaika zaidi hata siwezi kusikia; nimefazaika hata siwezi kuona.