Isaiah 22:14 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Mwenyezi-Mungu wa majeshi alinifunulia haya akisema: “Hakika hawatasamehewa uovu huu, watakufa bila kusamehewa. Mimi Mwenyezi-Mungu wa majeshi nimesema.”
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Mwenyezi Mungu, Mungu wa majeshi ya mbinguni amelifunua hili nikiwa ninasikia: Mwenyezi Mungu, Mungu wa majeshi ya mbinguni, asema: “Hadi siku ya kufa kwenu, dhambi hii haitafanyiwa upatanisho.”
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Na yeye Bwana wa majeshi akafunua haya masikioni mwangu, Ni kweli, uovu huu hautatakaswa wala kuwatokeni hata mfe; asema Bwana, Bwana wa majeshi.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Mwenyezi-Mungu wa majeshi alinifunulia haya akisema: “Hakika hawatasamehewa uovu huu, watakufa bila kusamehewa. Mimi Mwenyezi-Mungu wa majeshi nimesema.”
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
BWANA Mwenye Nguvu Zote amelifunua hili nikiwa ninasikia: Bwana, BWANA Mwenye Nguvu Zote, asema: “Mpaka siku ya kufa kwenu, dhambi hii haitafanyiwa upatanisho.”
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
bwana Mwenye Nguvu Zote amelifunua hili nikiwa ninasikia: Bwana, bwana Mwenye Nguvu Zote, asema: “Mpaka siku ya kufa kwenu, dhambi hii haitafanyiwa upatanisho.”
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Na yeye BWANA wa majeshi akafunua haya masikioni mwangu, Ni kweli, uovu huu hautatakaswa wala kuwatokeni hata mfe; asema Bwana, BWANA wa majeshi.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Mwenyezi-Mungu wa majeshi alinifunulia haya akisema: “Hakika hawatasamehewa uovu huu, watakufa bila kusamehewa. Mimi Mwenyezi-Mungu wa majeshi nimesema.”
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Kwa hiyo Bwana Mwenye vikosi ameyafumbua masikioni mwangu: Mpaka mtakapokufa, hamtaondolewa kabisa manza hizi, mlizozikora. Ndivyo, anavyosema Bwana Mungu Mwenye vikosi.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Na yeye BWANA wa majeshi akafunua haya masikioni mwangu, Ni kweli, uovu huu hautatakaswa wala kuwatokeni hata mfe; asema Bwana, BWANA wa majeshi.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
Yawe wa majeshi alinifunulia haya akisema: Hakika uovu huu hautasahauliwa mbele ya kufa kwenu. Ni Yawe wa majeshi anayesema hivyo.