Isaiah 22:18 — Compare Translations
11 translations compared side by side
Swahili (BHN) (Habari Njema) 2001
Atakubana kabisa na kukuzungushazungusha, kisha atakutupa kama mpira mpaka katika nchi pana. Huko utafia karibu na magari yako ya vita unayojivunia. Wewe ni aibu kwa nyumba ya bwana wako.
Swahili (Neno: Maandiko Matakatifu 2024)
Atakuvingirisha uwe kama mpira na kukutupa katika nchi kubwa. Huko ndiko utakakofia, na huko ndiko magari yako ya vita ya fahari yatabakia, na kuwa fedheha kwa nyumba ya bwana wako!
Swahili (SRUV) (Swahili Revised Union Version)
Hakika atakukunja na kukutupa kama mpira, mpaka nchi iliyo mbali; huko utakufa, na magari ya utukufu wako yatakuwa kuko huko, ewe uliye aibu ya nyumba ya bwana wako.
Swahili BHNTLK (Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza)
Atakubana kabisa na kukuzungushazungusha, kisha atakutupa kama mpira mpaka katika nchi pana. Huko utafia karibu na magari yako ya vita unayojivunia. Wewe ni aibu kwa nyumba ya bwana wako.
Swahili NEN (Neno: Bibilia Takatifu 2025)
Atakuvingirisha uwe kama mpira na kukutupa katika nchi kubwa. Huko ndiko utakakofia, na huko ndiko magari yako ya vita ya fahari yatabakia, wewe unayeifedhehesha nyumba ya bwana wako!
Swahili NMM (Neno: Maandiko Matakatifu) 2018
Atakuvingirisha uwe kama mpira na kukutupa katika nchi kubwa. Huko ndiko utakakofia, na huko ndiko magari yako ya vita ya fahari yatabakia, wewe unayeifedhehesha nyumba ya bwana wako!
Swahili RSUVDC (BIBLIA KISWAHILI)
Hakika atakukunja na kukutupa kama mpira, mpaka nchi iliyo mbali; huko utakufa, na magari ya utukufu wako yatakuwa huko huko, ewe uliye aibu ya nyumba ya bwana wako.
Swahili SCLDC10 (BIBLIA Yenye Vitabu vya Deuterokanoni HABARI NJEMA)
Atakubana kabisa na kukuzungushazungusha, kisha atakutupa kama mpira mpaka katika nchi pana. Huko utafia karibu na magari yako ya vita unayojivunia. Wewe ni aibu kwa nyumba ya bwana wako.
Swahili SRB37 (Swahili Roehl Bible 1937)
Atakuzinga, uviringane kama mpira, akutupe katika nchi iliyopanuka pande mbili; ndiko, utakakokufa, ndiko, magari yako mazuri yatakakokufuata wewe uliyeitweza Nyumba ya Bwana wako.
Swahili SUV (Maandiko Matakatifu ya Mungu Yaitwayo Biblia)
Hakika atakukunja na kukutupa kama mpira, mpaka nchi iliyo mbali; huko utakufa, na magari ya utukufu wako yatakuwa kuko huko, ewe uliye aibu ya nyumba ya bwana wako.
Swahili SWC02 (BIBLIA Maandiko Matakatifu Kwa Watu Wote 2002)
na kukuzungushazungusha, kisha atakutupa kama mupira mpaka katika inchi pana. Huko utakufia karibu na magari yako ya vita unayojivunia, wewe unayezaraulisha nyumba ya bwana wako.